
Bobi Wine amtaka Jaji Mkuu kutosikiliza shauri lake
Got a TV Licence?
You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.
Find out moreMuhtasari
- Mahakama ya Rwanda kuanza kusikiliza kesi ya Paul Rusesabagina
- Bobi Wine amtaka Jaji Mkuu kutosikiliza shauri lake
Habari za moja kwa moja
Na Lizzy Masinga
time_stated_uk
Mahakama ya Rwanda kuanza kusikiliza kesi ya Paul Rusesabagina
Copyright: BBCImage caption: Paul Rusesabagina Mahakama ya Rwanda hii leo inaanza kusikiliza kesi dhidi ya Paul Rusesabagina nawengine 20 ambao wanakabiliwa na mashtaka ya ugaidi.
Rusesabagina,mkosoaji wa Rais Paul Kagame, anatuhumiwa kuunga mkono shughuli za kikosiNational Liberation (FLN), ambaco ni mrengo wa wanamgambo wa chama chake chaRwandan Movement for Democratic Change (MRCD).
Copyright: BBCImage caption: Paul Rusesabagina akiwa Mahakamani Alikamatwa mnamo Agosti 2020 akiwa katika nchi ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na kurudishwa nchini Rwanda kukabiliana na mashtaka ya ugaidi, utekaji nyara na mauaji.
Mwezi Julai mwaka 2018, FLN ilidai kuhusika na mashambulio katika mkoa wa kusini wa Rwanda.
Copyright: BBCRusesabagina alifahamika kufuatia filamu ya Hotel Rwanda ikielezea jinsi alivyookoa maisha ya watutsi waliokuwa wamekimbilia katika hoteli moja mjini Kigali aliyokuwa meneja wake mwaka 1994.
Rais Paul Kagame amesema kikubwa sio ushujaa wa Bwana Rusesabagina au vitendo vyake wakati wa mauaji ya kimbari akisema kinachoangaliwa kwa sasa ni yeye.
Bwana Kagame amesema kwamba hajali kuhusu hadithi ya Bwana Rusesabagina kwamba yeye ni shujaa wa mauaji ya kimbari na kwamba ''hilo si jambo ambalo litakalomkabili mahakamani''.
"Kuna maswali ambayo lazima atayajibu.kuna wanaomsaidia wakiwa Ulaya,Marekani na kwIngineko na ambao walimpandisha cheo na kumpa majina ya ushujaa.awe shujaa au la ,mimi sina wasi wasi na hilo.
Copyright: BBCImage caption: Balozi wa Marekani nchini Rwanda akiingia mahakamani kusikiliza kesi hiyo Bobi Wine amtaka Jaji Mkuu kutosikiliza shauri lake
Copyright: Getty ImagesKiongozi wa upinzani RobertKyagulanyi maarufu Bobi Wine , amemtaka jaji Mkuukujiondoa katika kusikiliza shauri la kupingakuchaguliwa tena Rais Yoweri Museveni.
Bobi Wine amemshutumujaji Alfonse Owiny- Dollo kwa upendeleo kwa sababu ya ushirika wake na rais.
Mwanasiasa wa upinzanipia anataka majaji wengine wawili wa mahakama ya juu kujiondoa kusikilizashauri hilo kwa misingi hiyo hiyo.
Majaji watatuhawajajibu chochote kuhusu shutuma dhidi yao.
Jaji Mkuu Owiny-Dolloalikuwa mwanasheria wa Rais Museveni mwaka 2006, kwa mujibu wa tovuti ya NilePost.
Jaji Mike Chibitaalikuwa msaidizi wa Museveni katika masuala ya sheria, wakati Jaji EzekielMuhanguzi ni ndugu wa Waziri wa Ulinzi Elly Tumwine kwa mujibu wa vyombo vyahabari vya nchini humo.
Bobi Wine amedai kuwawatatu hao hawataweza kutenda haki iwapo watasikiliza shauri hilo.
Habari! karibu katika matangazo ya moja kwa moja ya taarifa zetu

Formed in 2009, the Archive Team (not to be confused with the archive.org Archive-It Team) is a rogue archivist collective dedicated to saving copies of rapidly dying or deleted websites for the sake of history and digital heritage. The group is 100% composed of volunteers and interested parties, and has expanded into a large amount of related projects for saving online and digital history.







