Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Ziwa Van

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani ya Ziwa Van
Ziwa Van pamoja na kanisa kwenye kisiwa cha Akdamar

Ziwa Van (kwaKituruki: Van Gölü; kwaKikurdi: Gola Wanêkwa; kwaKiarmenia: Վանա լիճ, Vana lič̣) niziwa kubwa la chumvi naziwa kubwa zaidi nchiniUturuki,mashariki mwa nchi.

Jiografia

[hariri |hariri chanzo]

Ziwa Van iko katikanyanda za juu kwenyekimo chamita 1,640. Linapokeamaji yake kutokamilima jirani lakini hakuna njia ya maji kutoka;mto uliotoka zamani ulifungwa namiamba yavolkeno miakamilioni iliyopita.

Umbali kati yamijiTatvan upande wamagharibi naVan upande wa mashariki nikilomita 93, umbali mkubwa wa magharibi hadi mwisho wahori upande wa mashariki ni km 127. Umbali mkubwa kutokakaskazini hadikusini ni km 52.

Kina kirefu nimita 451.

Kunaferi yareli inayozunguka baina ya Tatvan na Van.Treni za kimataifa baina ya Uturuki naIran zinavuka hapa.

Chumvi na ekolojia

[hariri |hariri chanzo]

Maji yake ni yachumvichumvi, takriban nusunusumagadi naNaCl. Maji huwa kwawastani nathamani pH ya 9.8.[1]

Kiwango cha magadi kwenye ziwa kinabadilika kufuatana namajira, pia ni tofauti kufuatana na kina cha maji. Maji yenye chumvi nyingi ni mazito zaidi, hivyo maji ya usoni hayana magadi mengi sawa na maji ya chini. Pia sehemu karibu naufuko ambako mito inaingia huwa na maji matamu kuliko eneo la katikati.

Kunaspishi moja yasamaki pekee (alburnus tarichi) inayopatikana katika ziwa; wakati wa kuzaa wanarudi kwenye midomo ya mito ambako kiasi cha maji matamu ni cha juu zaidi, baadaye wanaweza kurudi katika sehemu ambako kiwango cha magadi ni juu kiasi.

Kuna aina nyingi zaplanktoni.

Ramani inaonyeshalugha za mazingira ya Ziwa Van kabla yamaangamizi ya Waarmenia; kibichi ni wasemaji waKiarmenia, njano ni Wakurdi.

Historia na utamaduni

[hariri |hariri chanzo]

Katikamilenia ya kwanza KK Ziwa Van lilikuwa sehemu yamilki ya Urartu.

Tangukarne ya 3 KK Ziwa Van lilikuwa katikati ya maeneo yaliyokaliwa naWaarmenia. Ushuhuda wake hadi leo nimonasteri yaKiarmenia kwenyekisiwa chaAkdamar. Tangumaangamizi ya Waarmenia taifa hilo halipo tena hapa lakiniwatalii wengi Waarmenia wanatembelea Akdamar.

Siki hizi kunaWakurdi wengi katika mazingira ya ziwa.

Marejeo

[hariri |hariri chanzo]
  1. Andreas Reimer, Günter Landmann & Stephan Kempe, Lake Van, Eastern Anatolia, hydrochemistry and history. Aquatic Geochemistry 15: 195-222, 2009

Tovuti za Nje

[hariri |hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Ziwa_Van&oldid=1337596"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp