Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Ziwa Kyoga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ziwa Kyoga
{{{maelezo_ya_picha}}}
{{{maelezo_ya_picha}}}
Mahali{{{mahali}}}
Nchi zinazopakana{{{nchi}}}
Eneo la maji{{{eneo}}}
Kina cha chini{{{kina}}}
Mito inayoingia{{{mito inayoingia}}}
Mito inayotoka{{{mito inayotoka}}}
Kimo cha uso wa maji
juu yaUB
{{{kimo}}}
Miji mikubwa ufukoni{{{miji}}}

Ziwa Kyoga (pia huandikwaKioga) niziwa kubwa lenyekina kifupi katikaUganda, karibuKm² 1,720 kwa eneo na mwinuko wamita 914 juu yausawa wa bahari.

MtoViktoria Nile hupitia katika ziwa hili katika njia yake kutokaZiwa Viktoria na kuelekeaZiwa Albert. Chanzo kikuu kutoka Ziwa Viktoria hudhibitiwa naKituo cha stima cha Nalubaale katikaJinja. Chanzo kingine cha maji ni kanda yaMlima Elgon kwenye mpaka kati ya Uganda naKenya. Hata kama Ziwa Kyoga ni sehemu ya mfumo waMaziwa Makuu ya Afrika, halichukuliwi kama ziwa kuu.

Mito na maziwa ya Uganda. Bonyeza ili kukuza picha.

Upeo wa kina cha ziwa huwa karibu mita 5.7, na karibu lote huwa chini ya m 4. Maeneo chini m 3 huwa namimea ya maji, wakati eneo kubwa lapwanikinamasi huwa napapyrus namimea ya majini.Mimea hii pia huundavisiwa vinavyootea ambavyo husonga katikati yavisiwa vidogo vya kudumu. Maeneo yaliyo na maji ambayo hutoa maji kutoka mito huzunguka ziwa hili.

Ziwa la jirani niZiwa Kwania ambalo ni ziwa dogo lakini lenye kina kirefu.

Aina 46 zasamaki wametambulika katika Ziwa Kyoga, namamba ni wengi.

Mvua kubwa zaEl Nino katika miaka 1997-1998 zilisababisha ngazi za juu za maji, na kuzidisha ukuaji wa papyrus na mimea ya majini`ambayo iliunda mikeka na kufungamdomo waVictoria Nile. Kufungana huku kulisababisha ngazi ya maji kupanda juu zaidi, mafuriko karibu 580 km ² za ardhi iliyozunguka eneo hili(DWD 2002) na kusababisha watu kukimbia makazi yao na uharibifu wa uchumi. Mwaka wa 2004, serikali yaMisri ilitunza Ugandadolamilioni 13 kwa kurekebisha mtiririko wa mto Nile katika Ziwa Kyoga.

Marejeo

[hariri |hariri chanzo]
  • DWD (2002)Utayarishaji wa El Nino katika Ziwa Kyoga na maeneo mengine yanayofurika nchini Uganda. Kurugenzi ya Maji na Maendeleo. Wizara ya Maji, Ardhi na Mazingira, Entebbe, Uganda.
  • Ilm (2004)kusaidia katika Usimamizi wa k Sudd katika Ziwa Kyoga. Iliyotolewa na Mradi wa Mazingira ya Ziwa na Kituo cha Mazingira cha Finland, EIA Ltd(Toleo la PDF kwenye mtandao)
  • Twongo, T. (2001)uvuvi na mazingira ya Maziwa ya Kyoga .Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi (FIRRI), Jinja, Uganda.
  • Kumbukumbu ya Maziwa Duniani kiingilio cha Ziwa KyogaIlihifadhiwa 23 Mei 2011 kwenyeWayback Machine.

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]
Maziwa


Makala hii kuhusu maeneo yaUganda bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusuZiwa Kyoga kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Ziwa_Kyoga&oldid=1146722"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp