Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Zheng He

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu ya kisasa ya Zheng He.

Zheng He (pia:Cheng Ho;1371-1433) alikuwabaharia,kiongozi wa kijeshi nampelelezi kutokaChina wakati wanasaba ya Ming. Akiwa mkuu wajeshi la maji la China aliongoza misafara yamajahazi yake hadipwani zaAfrika hadiMsumbiji akapelelezaBahari Hindi navisiwa vyaAsia ya Kusini-Mashariki.

Maisha yake

[hariri |hariri chanzo]

Zheng He alizaliwa kwajina la Ma He katikafamilia yaWachina Waislamu kwenyejimbo laYunnan[1].Baba yake aliwahi kusafiriMaka kwahajj.

Alipozaliwa Yunnan ilikuwa chini yautawala waWamongolia lakini mnamomwaka1381jeshi la Ming lilivamia na kuteka Yunnan. Kwenyevita hiyokijana alikamatwa kama mfungwa akafikishwa kwenyemakao makuu yaKaisari wa China. Huko alihasiwa kuwatowashi jinsi ilivyokuwa kawaida kwawatumishi wawafalme huko China[2].

Alikuwarafiki wamtoto wa Kaisari akafundishwa mengi pamoja naye. Huyo alipokuwa Kaisari mwenyewe kwa jina laYongle alimpamadaraka juu yajeshi la maji[3] .

Twiga kutokaMalindi alifika China kwameli za Zheng He.

Safari

[hariri |hariri chanzo]

Kati ya miaka1405 na1433 Zheng He aliongoza misafara 7 zabaharini kama kiongozi wa vikundi vikubwa vyameli. Meli zake zilikuwa majahazi makubwa sana yaliyobeba haditani 1500. Kilasafari Zheng He alipewa meli 50-60 naidadi yawanajeshi na mabaharia ilikuwa takriban 25,000 - 30,000.

Meli za Zheng He kwenye picha ya Kichina yakarne ya 16.

Safari tatu za kwanza zilipeleleza maeneo yanayoitwa leoIndonesia,Uhindi naSri Lanka. Katika safari za tatu hadi saba aliendelea hadi pwani za Afrika.

Miaka14131415 alisafiri mara ya kwanzaAfrika ya Mashariki. AlitembeleaMogadishu naMalindi kwenye pwani yaKenya.Sultani wa Malindi alimtumabalozi na meli za Zheng He aliyeletatwiga kamazawadi kwa Kaisari wa China.Mnyama huyo alisababisha Wachina kushangaa na kuna picha yake iliyochorwa wakati ule.

Kufika hadi Atlantiki na Amerika?

[hariri |hariri chanzo]

Wataalamu kadhaa wamedai ya kwamba kwenye safari ya1421kundi dogo la meli zake liliingiaAtlantiki na kuivuka hadi kufikaAmerika. Lakini hii inapingwa na wataalamu wengi.

Hata hivyo kunaramani yadunia yaMwitaliaFra Mauro ya mwaka1459 aliyechora meli ya Kichina katika Atlantiki pamoja na maelezo ya kwamba yeye alipata habari kuhusu meli kubwa kutokamashariki iliyoingia Atlantiki. Maelezo yale hayaeleweki kabisa kwa sababu wakati uleWareno walikuwa hawajafika bado kusini mwa Afrika wala hawakuingia Bahari Hindi bado na Amerika haikujulikana, hivyo Fra Mauro hakuwa na majina kwa yale aliyosikia.

Zheng alikufa ama wakati wa safari yake ya mwisho au mara moja baada ya kurudi akazikwa karibu namji waNanjing.

Mwisho wa safari

[hariri |hariri chanzo]

Makaisari wa baadaye walisimamisha safari. Mitindo wa Zheng He ilikuwa nagharama kubwa sana. Yote ililipiwa naserikali kuu na gharama zilipitafaida yabidhaa zilizoletwa. Tofauti na safari za Wareno naWahispania waliofika Amerika, Afrika Mashariki na Uhindi miaka 60 baada ya Zheng He, China haikutafuta faida ya kiuchumi katika upelelezi wake na pia haikutambua nafasi zabiashara katika nchi hizo za mbali.

Meli kubwa za Zheng He zilifungwabandarini zikaoza polepole.

Marejeo

[hariri |hariri chanzo]
  1. J. V. G. Mills (1970).Ying-yai Sheng-lan, The Overall Survey of the Ocean's Shores (1433), translated from the Chinese text edited by Feng Ch'eng Chun with introduction, notes and appendices by J. V. G. Mills. White Lotus Press. uk. 5.ISBN 974-8496-78-3.
  2. Edward L. Dreyer (2007).Zheng He: China and the Oceans in the Early Ming, 1405–1433. Longman. uk. 12.ISBN 0-321-08443-8.
  3. Tsai, Shih-shan Henry. "Zheng He." World Book Student. World Book, 2013. 4 December 2013.

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Zheng_He&oldid=1186815"
Jamii:
Jamii iliofichwa:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp