Zeu |
---|
 Kichwa cha sanamu ya Zeu |
Mkuu wa miungu Mungu wa Mbingu na Radi |
Makao | Mlima Olimpos |
---|
Alama | Radi,Tai,Fahali naMwaloni |
---|
Mwenzi | Hera |
---|
Wazazi | Kronos naRhea |
---|
Ndugu | Hestia,Hades,Hera,Poseidon naDemetra |
---|
Watoto | Ares,Athena,Apolo,Artemi,Afrodita,Dioniso,Heba,Herme,Herakle,Helena,Hefesto,Perseo,Minos,Muza Tisa |
---|
Ulinganifu wa Kirumi | Jupiter |
---|
Ulinganifu wa Kietruski | Tinia |
---|
Ulinganifu wa Kinorsi | Odin |
---|
|
Zeu (piaZeus kutokaKigiriki:ΖεύςZeus) ni mkuu wamiungu katikadini ya Ugiriki ya Kale. Analingana naJupiter katikadini ya Roma ya Kale. Katikaimani ya Wagiriki alikalia kilele cha mlima Olimpos pamoja na miungu wenzake alkini alikuwa mkuu na mwenye nguvu kushinda wengine.
Katika masimulizi ya Wagiriki alikuwa mtoto wa miungu Kronos na Rhea na mdogo wa Hestia, Demeter, Hera, Hades na Poseidon. Huyu baba-mungu Kronos alimeza watoto wake wote mara baada ya kuzaliwa akihofia ya kwamba watampindua sawa jini yeye mwenyewe aliwahi kumpindua babake mungu Uranos. Zeu alipoelekea kuzaliwa mamake Rhea alimficha pangoni akampa Kronos badale yake jiwe lililofunikwa na nguo akameza. Zeu alikua haraka akawa mkubwa na hapo alitumia mbinu wa dawa kumlazimisha baba kutapika watoto wote aliowahi kumeza. Baadaye aliungana na wakubwa zake na pamoja walimshambulia Kronos na kumshinda. Sasa miungu waliamua kugawana madaraka; Zeu alikuwa mungu mkuu wa mbinguni, Poseidon mkuu wa bahari na vilindi vyake na Hades mkuu wa dunia ya chini.
Zeu alimwoa dadake Hera akazaa watoto naye lakini alitoroka mara kwa mara kufanya mapenzi na miungu wa kike wengine au na mabinti wa kibinadamu; mitholojia ya Wagiriki ilitaja zaidi ya majina 30 ya miungu au mabinti aliozaa nao.
Aliheshimiwa na Wagiriki wote na kuabudiwa katika mahali pa pekee; pamoja na mahekalu kulikuwa na sehemu za misitu penyemiti iliyotazamiwa kuwa miti mitakatifu yake. Kisiwani Kreta waliabudu kwenye mipango aliposemekana kufichwa na mamake.
 | Makala hii kuhusu mambo ya dini bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari. |