Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Zenoni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Zenoni
Jina la ElementiZenoni
AlamaXe
Namba atomia54
Mfululizo safuGesi adimu
Uzani atomia131.293
Ugumu (Mohs){{{ugumu}}}
Kiwango cha kuyeyuka161.4K (-111.7°C)
Kiwango cha kuchemka165.03 K (-108.12 °C)
Asilimia zaganda la dunia2 · 10-9 %
Hali maadagesi

Zenoni ( kut.kigiriki ξένοςksenos “kigeni” kwa sababu wafumbuzi wa kwanza waliikuta mahali wasipoitegemea) nielementi yenyenamba atomia54 kwenyemfumo radidia nauzani atomia 131.293. Alama yake niXe.

Tabia

[hariri |hariri chanzo]

Ni gesi adimu inayopatikana katikaangahewa haina rangi wala herufu. Kama gesi adimu zote ni bwete na kutomenyuka kirahisi na kitu kingine;

Matumizi

[hariri |hariri chanzo]

Matumizi yake ni hasa katika aina mbalimbali za taa kwa sababu inasaidia balbu kuwa na mwanga mkali zaidi. Magari ya kisasa mara nyingi hutumia balbu za Zenoni zinatotoa mwanga mkali kwa matumizi madogo ya umeme.

Zenoni hutumiwa pia kwa vyombo vya angani kama kisukumaji. Kama gesi bwete haimenyuki na tangi na mapipa; kwa kanieneo kubwa hukaa thabiti kama kiowevu hadi halijoto ya chumbani; inageuzwa rahisi kuwa tena gesi kwa ajili ya injini.

Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Zenoni&oldid=1372426"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp