Waanzilishi wa YouTube.kulia ni Chad Hurley, Steve Chen na kushoto ni Jawed Karim
YouTube nitovuti ya kushirikishavideo ambazo watumiaji wanaweza kuzinakili na kuzigawa kwa wengine.Wafanyakazi watatu wa zamani waPayPal waliunda YouTube mnamoFebruari2005.[1]
MnamoNovemba2006,YouTube, LLC ilununuliwa naGoogle Inc kwaDolabilioni 1.65, na sasa huendeshwa kama shirika dogo la Google.Kampuni hii ipoSan Bruno,California na inatumiateknolojia yaAdobe Flash kuonyesha aina mbalimbali za video zilizotengenezwa na watumiaji, pamoja na vijisehemu vyasinema, vijisehemu vya maonyesho yaruninga, na video zanyimbo, vilevile maudhui ambayo hayajakomaa kama vile video za kublogu na video za asili zilizo fupi.
Ikoni kamili ya rangi ya YouTube
Maudhui mengi yaliyomo kwenye YouTube yametumiwa na watu binafsi, ingawavyombo vya habari pamoja na makampuni yakiwemoCBS,BBC,UMG na mashirika mengine hutoa baadhi yahabari zao, kama sehemu ya mpango waushirikiano na YouTube.[2]
Watumiaji ambao hawajasajiliwa wanaweza kutazama video, wakati watumiaji waliosajiliwa wanaruhusiwa kutumia na kunakiliidadi isiyo na kipimo ya video. Video ambazo zanaweza kuwa na maudhui yaliyo naujumbe wenyelugha isiyoruhusiwa zinapatikana kwa watumiaji waliosajiliwa tu na wenyeumri zaidi ya miaka 18. Kunakili kwa video zenye lugha ya kukashifu, mambo yangono, ukiukwaji wahakimiliki, na habari zinazohimizauhalifu kumepigwa marufuku katikamkataba wa masharti yahuduma ya YouTube.
Akaunti za watumiaji waliosajiliwa hujulikana kama "channels".[3]
Makao makuu ya sasa ya YouTube mjini San Bruno, California.
YouTube ilianzishwa naChad Hurley,Steve Chen naJawed Karim ambao awali wote walikuwa wafanyakazi waPayPal.[4] Hurley alisomea urasimu katika Chuo Kikuu cha Indiana ya Pennsylvania, huku Chen na Karim wakisomea kompyuta sayansi pamoja katikaChuo Kikuu cha Illinois huko Urbana-Champaign.[5]
Kulingana na hadithi inayorudiwa mara nyingi katika vyombo vya habari, Chad Hurley na Steve Chen waliibua wazo la YouTube wakati wa miezi ya mwanzo ya 2005, baada ya kukabiliana na matatizo ya kugawa video zilizochukuliwa kweye chakula cha jioni nyumbani kwa Chen hukoSan Francisco. Jawed Karim hakuhudhuria sherehe hii na alikana kwamba sherehe ilikuwepo, na Chad Hurley alisema kuwa, wazo kuwa YouTube lilianzishwa baada ya chakula cha jioni" pengine lilitiwa nguvu sana na mawazo ya matangazo ili kuunda hadithi yenye kueleweka zaidi."[6]
YouTube ilianza kama teknolojia ya kufadhiliwa, hasa kutoka kwa uwekezaji wa dola za Marekani milioni 11.5 kutoka kwaSequoia Capital kati ya Novemba 2005 na Aprili 2006.[7] Hapo awali makao makuu ya YouTube yalikuwa upande wa juu waPizzeria na mkahawa wa Kijapani katikaSan Mateo, California.[8] Jina la kikoa chakewww.youtube.com kilianza kutumika tarehe 15 Februari 2005, na tovuti iliundwa miezi kadhaa iliyofuata.[9] Video ya kwanza kwenye Youtube ilikuwaMe at the Zoo, na mwanzilishi wa onyesho Jawed Karim kwenyeSan Diego Zoo.[10] Video hii ilipakiwa mnamo tarehe 23 Aprili 2005, na bado yaweza kutazamwa kwenye tovuti.[11]
YouTube iliupatia umma toleo la kwanza la tovuti Mei 2005, miezi sita kabla ya uzinduzi rasmi mnamo Novemba 2005. Tovuti ilikua haraka, na Julai 2006 kampuni ilitangaza kwamba zaidi ya video mpya 65,000 zilikuwa zikipakiwa kila siku, na kwamba tovuti ilikuwa ikipokea watazamaji wa video milioni 100 kwa siku.[12] Kulingana na tarakimu zilizochapishwa na kampuni ya utafiti wa masoko comScore, YouTube inaongoza katika utoaji wa video kwenye mtandao katikaMarekani, ikiwa na mgawo wa soko wa karibu asilimia 43 na zaidi ya video bilioni sita zilizotazamwa mnamo Januari 2009.[13] Inakadiriwa kuwa video mpya za jumla ya masaa 20 hupakiwa kwa tovuti kila dakika, na kwamba karibu robo tatu ya nyenzo hizi hutoka nje ya Marekani.[14][15] Pia inakadiriwa kwamba katika mwaka 2007 YouTube ilitumiwa kipimo data sawa na kiasi kilichotumika kwenyewavuti mzima wa mwaka 2000.[16] Mwezi Machi 2008, kipimo data cha YouTube kiligharimu dola milioni 1 za Marekani kwa siku.[17]Alexa ameipa nafasi ya nne YouTube kama tovuti iliyotumiwa kwa wingi kwenye wavuti, nyuma yaGoogle,Yahoo! naFacebook.[18]
Uchaguzi wa jinawww.youtube.com ulisababisha matatizo kwa vile jina hili lilikuwa likitumika kwa tovuti,www.utube.com. Mmiliki wa tovuti, Universal Tube& Rollform Equipment, aliandikisha kesi mahakamani dhidi YouTube Novemba 2006 baada ya kupokea idadi kubwa ya watu waliokuwa wakitafuta YouTube. Universal Tube kwa sasa imebadilisha jina la tovuti yake na kuwawww.utubeonline.com.[19][20]
Mnamo Oktoba 2006,Google Inc ilitangaza kwamba ilikuwa imeipata YouTube kwadola bilioni 1.65 katika hisa za Google, agano hili lilikamilishwa tarehe 13 Novemba 2006. Google huwa haitoi tarakimu za kina za gharama ya kutunza YouTube, na mapato ya YouTube ya mwaka 2007 yalibainishwa kuwa "siyo kitu" katika uwekaji jalada. Juni 2008 nakala katika gazeti laForbes lilitoa makadirio ya mapato ya 2008 kuwa dola milioni 200 za Kimarekani, huku likibaini mafanikio katika mauzo ya matangazo.
Mnamo Novemba 2008, YouTube ilifikia makubaliano naMGM,Lions Gate Entertainment naCBS ambazo ziliruhusu makampuni kutuma filamu nzima na maonyesho ya televisheni kwenye tovuti, yakiandamana na matangazo. Hatua hii imekusudiwa kutoa ushindani kwa tovuti kamaHulu, ambazo huwa na nyenzo kutoka kwaNBC,Fox, naDisney.[21][22]
Tarehe 9 Oktoba 2009, wakati wa ukumbusho wa tatu kutoka kuchukuliwa naGoogle, Chad Hurley alitangaza katika chapisho la blogu ya kwamba YouTube ilikuwa inatumiwa na "zaidi ya watazamaji bilioni moja" duniani kote.
Kabla ya uzinduzi wa YouTube mwaka 2005, kulikuwa na mbinu chache rahisi zilizokuwemo kwa watumiaji wa kompyuta wa kawaida ambao walitaka kuchapisha video kwenye wavuti. Pamoja na kusano lake rahisi, YouTube ilirahisisha uwezekano wa mtu yeyote aliyeunganishwa kwa wavuti kuchapisha video ambazo watazamaji duniani kote wanaweza kutazama kwa muda wa dakika chache. Mada tofauti zilizoko katika YouTube zimegeuza ugawi wa video kuwa mojawapo ya sehemu muhimu ya utamaduni wa wavuti.
Mfano wa awali wa athari za kijamii za YouTube ulikuwa ufanisi wa video yaBus Uncle mwaka 2006. Inaonyesha mazungumzo makali kati ya kijana na mzee ndani ya gari la abiria huko Hong Kong, na ilijadiliwa sana katika wasimamizi wa vyombo vya habari vilivyoimarika.[23] Video nyingine iliyopokea uwambo niguitar,[24] ambayo ilihusisha uiigizi waPachelbel's Canon huku akiwa nagitaa laumeme. Jina la mwigizaji halijatolewa katika video, na baada ya kupokea mamilioni ya maoni gazeti laThe New York Times lilifichua jina la mcheza gitaa kamaJeong-hyun Lim, wa umri wa miaka 23 kutoka Korea ya Kusini ambaye alikuwa amerekodi traki hii ndani ya chumba chake cha malazi.[25]
YouTube ilipatiwa tuzo la 2008 laGeorge Foster Peabody na kunukuliwa kuwa " 'Uwanda wa Wasemi' " na iliyoonyesha na kukuza demokrasia."[26][27]
YouTube imekuwa ikilaumiwa kwa kushindwa kuhakikisha kwamba video zake zina heshimu sheria yahakimiliki. Wakati wa kupakia video,watumiaji wa YouTube huwa wanaonyesha daima kiwambo chenye ujumbe ufuatao:
Usipakie maonyesho yoyote ya televisheni, video za nyimbo, tamasha za miziki au ujumbe wa kibiashara bila ruhusa isipokuwa iwe maudhui yote yaliyomo uliyatengeneza wewe mwenyewe. Ukurasa wa vidokezo vya hakimiliki na Mwogozo wa Jumuiya unaweza kukusaidia kuamua kama video yako inakiuka hakimiliki za mtu mwingine.[28]
Lisha ya ushauri huu, bado kuna vijisehemu vingi vya maonyesho ya televisheni,video za nyimbo na filamu katika YouTube. YouTube huwa haitazami video kabla ya kuzichapisha kwenye wavuti, ila hupatia jukumu wamiliki wa hakimiliki kutoa notisi ya uvunjaji chini ya sheria zaMillennium Digital Copyright Act. Mashirika yakiwemoViacom, Mediaset naLigi kuu ya Uingereza yameandikisha kesi dhidi ya YouTube, yakidai kuwa imefanya juhudi kidogo mno kuzuia upakiaji wa nyenzo zenye hakimiliki.[29][30][31] Viacom, wanadai dola bilioni 1 za Kimarekani kama fidia yauharibifu, huku ikisema kuwa alikuwa imepata zaidi ya vijisehemu ambavyo vinatokana na nyenzo 150,000 zake katika YouTube na ambavyo vimetazamwa zaidi ya mara bilioni 1.5. YouTube alijibu kwa kusema ya kwamba huwa "inaenda mbali zaidi ya mipaka yake kisheria katika kusaidia kulinda nyenzo za wamiliki na kazi zao". Tangu Viacom kuandikisha kesi yake, YouTube imeanizisha mfumo uitwao VideoID, ambao huangalia video zilizopakiwa dhidi ya hifadhidata ya maudhui yenye hakimiliki kwa lengo la kupunguza ukiukaji.[32][33]
Mnamo Agosti 2008, mahakama ya Marekani iliamua ya kwamba wamiliki wa hakimiliki hawawezi kuagiza kuondolewa kwa faili iliyo katika wavuti bila kwanza kubainisha kuwa kupakiwa kwakwe kunaonyesha matumizi ya haki ya nyenzo hii[[]]. Kesi hii ilihusisha Stephanie Lenz kutokaGallitzin, Pennsylvania, ambaye alikuwa ameunda video ya kinyumbani ya mwanawe wa kiume wa miaka 13 huku akicheza wimbo waPrince "Let's Go Crazy" na kupakia video hii ya sekunde 29 kwa YouTube.[34]
Faragha
Mnamo Julai 2008,Viacom ilishinda uamuzi wa mahakama uliohitaji YouTube kutoa na kuipa data kuhusu tabia ya kila mtazamaji ambaye anatazama video kenye tovuti. Hatua hii ilisababisha wasiwasi kwamba tabia ya mtazamaji binafsi ingeweza kutambuliwa kwaanwani ya IP na majina yao ya kuingilia tovuti. Uamuzi huo ulitiliwa lawama naElectronic Frontier Foundation, ambayo iliita uamuzi huu wa mahakama kama "sera inayorundisha nyuma haki za ufaragha".[35] JajiLouis Stantonwa Mahakama ya Wilaya aliutupilia mbali wasiwasi wa faragha kama "uvumi", na kuiamuru YouTube kukabidhi nyaraka zilizokaribiaterabyte 12 za data. Jaji Stanton alikataa ombi la Viacom kwa YouTube kukabidhichanzo kanuni zamfumo wake wa utafiti, akisema kuwa hakuna ushahidi kuwa YouTube ilichukulia ukiukaji wa hakimiliki kwa namna tofauti.[36][37]
Maudhui yasiyofaa
YouTube pia imekabiliwa na upinzani juu ya maudhui ya kukera yaliyomo katika baadhi ya video zake. Ingawasheria ya utumiaji wa YouTube hukataza kupakia kwa video ambayo ina uwezekano wa kuwa na nyenzo zisizofaa, YouTube huwa haiangali kila video kabla ya kuwekwa kwenye wavuti. Sehemu zenye utata katika video zinahusishaukanaji wa Mauaji ya Holocaust na mkasa wa Hillsborough, ambapo mashabiki 96 kutokaLiverpool waliangamizwa mwaka wa 1989, kwenye njama za kidhahania na dini.[38][39]
YouTube hutegemea watumiaji wake kuonyesha ishara kuhusu maudhui ya video kama ni yale yasiyofaa, na wafanyakazi wa YouTube watatazama video iliyoashiriwa kubaini kama inakiukamkataba wa masharti ya utumizi wa tovuti.[3] Mnamo Julai 2008 Kamati ya Utamaduni na Vyombo vya habari yaBunge la Umoja la Uingereza ilisema ya kwamba ilikuwa "haijaridhishwa" na mfumo wa YouTube wa kutoa sera za video zake, na kujadili kuwa "kukabiliwa awali kwa maudhui yafaa kuwa kigezo cha sera ya tovuti kupakia [[maudhui yanayotoka kwa watumiaji|maudhui yanayotoka kwa watumiaji." YouTube alijibu kwa kusema kuwa: "Tuna sheria kali juu ya kile kinachoruhusiwa, na mfumo unaowezesha mtu yeyote ambaye anaona maudhui yasiyofaa kuripoti kwetu 24 / 7 kwa timu yetu na suala hili kushughulikiwa mara moja. Sisi huelimisha jamii yetu juu ya sheria na inahusisha kiungo cha moja kwa moja kutoka kwa kila ukurusa wa YouTube ili kurahisisha mchakato huu kama iwezekanavyo kwa watumiaji wetu. Kutokana na idadi kumbwa ya maudhui yaliyo pakiwa kwenye tovuti yetu, tunadhani kuwa hadi sasa hii ndiyo njia yenye ufanisi zaidi ili kuhakikisha kuwa video chache ambazo huvunja kanuni zinashuka haraka.[40]
Tarehe 3 Desemba 2006,Iran iliziba kwa muda upataji wa YouTube, pamoja na tovuti zingine kadhaa, baada ya kuzitangaza kama zinazokiuka maadili ya kijamii na kanuni za vitendo. YouTube ilizibwa baada ya video iliyopakiwa kwenye wavuti kujaribu kumwonyesha Mwajemi/Mwirani anayeiigiza katika filamu za mapenzi akishiriki katika ngono.[47] Kuzibwa huku baadaye kuliondolewa na kisha kukarejeshwaUajemi baada ya uchaguzi wa rais 2009.[48]
Mnamo 23 Februari 2008,Pakistan iliziba YouTube kutokana na "nyenzo za kukera" kwaimani ya Uislamu , pamoja na kuonyeshwa kwakatuni ya Kideni ya nabiiMuhammad.[49] Hii ilisababisha karibu kuzimwa kimataifa kwa tovuti ya YouTube karibu masaa mawili, kwa vile kuzibwa huko kwa Pakistan kulichukuliwa na nchi nyingine. Pakistan iliondoa kizibo chake tarehe 26 Februari 2008.[50] Wapakistani walizunguka kizibo hicho cha siku tatu kwa kutumiaprogramu mtandao wa kibinafsi. [[]].[51]
Shule katika baadhi ya nchi zimeziba upatikanaji wa YouTube kutokana na wanafunzi wa kupakia video zenye tabia ya uchokozi, vita vya shuleni,tabia ya ubaguzi wa rangi, na nyenzo zingine zisizofaa.[52]
Teknolojia
Ulinganifu wa kawaida, juu, na HD wa ubora wa video za YouTube zikichezwa katika YouTube na uimarisho wa asili wa video hizi.
Muundo wa video
Teknologia ya urejeshi wa kucheza Video za YouTube kwa watumiaji wa mtandao inatokana naAdobe Flash Player. Hii inaruhusu tovuti kuonyesha video bora ikilinganishwa na teknolojia zilizoimarika za kucheza video (kamaWindows Media Player, QuickTime, naRealPlayer) ambazo kwa ujumla huhitaji mtumiaji kupakua na kuwekaprogramu-jalizi kwa kivinjari ili kutazama maudhui ya video.[53] Kutazama video ya Flash pia kunahitaji plogramu-jalizi, lakiniutafiti wa soko kutoka kwaAdobe Systems umegundua ya kwamba plogramu-jalizi yake imewekwa kwa Kiwango cha asilimia 95 kwenye kompyuta za kibinafsi.[54]
Video zilizopakiwa kwa YouTube kutoka kwa wamiliki maalum wa akaunti zafaa kuwa na urefu wa dakika kumi na faili ya kiasi chaGB[55] 2.[56] Wakati YouTube ilipozinduliwa mwaka wa 2005 kulikuwa na uwezekano wa kupakia video ndefu, lakini upeo wa dakika kumi ulianzishwa Machi 2006 baada ya YouTube kugundua kwamba nyingi ya video zilizozidi urefu huu zilikuwa na maudhui yasiyoruhusiwa ya maonyesho ya televisheni na filamu.[57][58] Akaunti za ushirika zinaruhusiwa kupakiwa kwa video zenye urefu wa zaidi ya dakika kumi, lakini kwa kukubaliwa na YouTube.[59]
YouTube awali ilitoa video katika muundo mmoja tu, lakini sasa ina miundo mikuu mitatu, vilevile muundo wa "simu za mkononi", wa kutazamwa kwenyesimu za mkononi. Muundo asili, sasa una kibali cha "ubora wa wastani", huonyesha video kwa uimarisho wapixel 320x240 kwa kutumiaSpark Sorenson Codec, pamoja namono MP3 audio.[61] Hii ilikuwa, kwa wakati huo, kiwango cha wastani cha kutazama video kwenye wavuti.
Video za "ubora wa juu", zilizoanzishwa Machi 2008, huonyeshwa hadi kwa pixels 864x480 na sauti ya stereoAAC.[62] Muundo huu huwa na umuhimu mkubwa katika kuboresha kiwango cha wastani cha ubora. Mwezi Novemba 2008720p HD ya kuwezesha zaidi iliongezwa.[63] Wakati huo huo, kifaa cha kucheza video cha YouTube kilibadilishwa kutoka kwa4:3kipengele cha uwiano hadi kwakiwambo kipana.16:9Video za 720p huwa zinaonyeshwa kwa uimarisho wa pixel 1280x720, uimarisho huu ukiwa umetengenezwa naH.264 video Codec. Pia hili linahusisha stereo audio ikiwa imetengenezwa na AAC.
Utazamaji wa video kwa njia ya 3D
Katika video iliyochapishwa mnamo 21 Julai 2009,[64] mhandisi wa plogramu wa YouTube Peter Bradshaw alitangaza kuwa watumiaji wa YouTube sasa wangeweza kupakia video za aina ya3D. Video hizi zinaweza kutazamwa kwa njia ya kawaida, na miwani huvaliwa na watazamaji ili kupata athari ya 3D.[65][66][67]
Upatikanaji wa matini
Mojawapo ya sifa za YouTube ni uwezo wa watumiaji kutazama video zake katika tovuti nje ya wavuti wake. Kila video ya YouTube huandamana pamoja na kipande chaHTML, ambacho chaweza kutumika kuiweka kwenye ukurasa nje ya tovuti ya YouTube. Utendakazi huu mara nyingi hutumika kuweka video za YouTube katika kurasaza mitandao ya kijamii nablogu.[68]
YouTube kawaida huwa haitoi kiungo cha kupakua video zake, na hutarajia kuwa huwa zinatazamwa kupitia kwa kusano la tovuti yake.[69] Idadi ndogo ya video, kama vile hotuba ya raisBarack Obama, inaweza kupakuliwa kama faili zaMP4.[70] Wavuti mbalimbali za mrengo wa tatu, na vifaa vya matumizi naplogramu-jalizi za kivinjari huruhusu watumiaji kupakua video za YouTube.[71] Mnamo Februari 2009, YouTube ilitangaza huduma ya majaribio, ya kuruhusu baadhi ya washirika kutoa upakuaji wa video bure au kwa malipo ya ada kwa njia yaGoogle Checkout.[72]
Majukwaa
Baadhi yasimujanja zina uwezo wa kupata video za YouTube, kutegemea mtoaji na mpango wa data. Simu ya YouTube ilizinduliwa mwezi Juni 2007, na hutumiaRTSP ili kutazama video.[73] Si video zote za YouTube zinazopatikana kwenye muundo wa tovuti ya simu.[74]
Tangu Juni 2007,video za YouTube huwa zinapatikana kwa ajili ya kutazamwa katika bidhaa mbalimbali zaApple. Hii ilihitaji matini ya YouTube kubadilishwa hadi katika kiwango wastani kinachopendelewa cha Apple,H.264, mchakato uliochukua miezi kadhaa. Video za YouTube huweza kutazamwa kwa kutumia vifaa vikiwemoApple TV naiPhone.[75] Huduma yaTiVoiliyoboreshwa mnamo Julai 2008 iliruhusu mfumo huu kutafuta na kucheza video za YouTube.[76] Mnamo Januari 2009, YouTube ilizindua "YouTube ya TV", na ni toleo la tovuti ya inayolenga mfumo wa set-top boxes na vyombo vingine vya habari vinavyohusu vifaa vya TV vyenye vivinjari, mwanzo, zikiruhusu video zake kutazamwa katikaPlayStation 3 naWii video game console s.[77][78] Mwezi Juni 2009, YouTube XL ilitolewa, ambayo ina kusano iliyorahisishwa, iliyoundwa kwa ajili ya kutazama kwenye televisheni yenye kiwamgo cha wastani.[79]
Hivi karibuni imeanzishwa Youtube kwa lugha yaKiswahili.
Kusano la YouTube hupendekeza mfumo ambao unapaswa kuchaguliwa kwa kuzingatiaanwani ya IP ya mtumiaji. Katika baadhi ya matukio, ujumbe "Video hii haipatikani katika nchi yako" waweza kuonekana kutokana na vikwazo vya hakimiliki au maudhui yasiyofaa.[87]
Mipango ya YouTube ya kuunda toleo hukoUturuki imepatwa na matatizo, tangu mamlaka ya Kituruki ilipoihitaji YouTube kuanzisha ofisi huko Uturuki, ambayo ingekuwa chini ya sheria za Kituruki. YouTube anasema kwamba haina nia ya kufanya hivyo, na kwamba video zake haziko chini ya sheria za Kituruki. Mamlaka ya Kituruki yameonyesha wasiwasi kuwa YouTube imetumika kupakia video zenye matusi kwaMustafa Kemal Atatürk na baadhi ya nyenzo zake ni zakukera kwaWaislamu[88][89]
Mwezi Machi 2009, mabishano kati ya YouTube na wakala wa ukusanyaji wa asilimia ya mapato ya muziki[[]] Uingereza [[]]PRSP walisababisha video za premia kuzibwa kwa watumiaji wa YouTube nchiniUingereza. Kuondolewa kwa video zilizopakiwa na makampuni makubwa ya kurekodi kulitokea baada ya kushindwa kufikia makubaliano juu ya mpango wa leseni. Mgogoro huu ulitatuliwa Septemba 2009.[90] Mwezi Aprili 2009, mzozo kama huo ulisababisha kuondolewa kwa video za nyimbo zenye kulipiwa kwa watumiaji kutokaUjerumani.[91]
↑Colley, Andrew (2007-03-06)."States still hold out on YouTube". Australian IT. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutokachanzo mnamo 2009-02-23. Iliwekwa mnamo2009-12-01.{{cite news}}:Text "accessdate2007-10-11" ignored (help)