| Yosefina Bakhita | |
|---|---|
![]() | |
| Amezaliwa | 1869, Algozney, Darfur, Sudan |
| Anaheshimiwa na | Kanisa Katoliki |
| Feast | {{{feast_day}}} |
Yosefina Margaret Bakhita,F.D.C.C., (Algozney,Darfur[1]1869 hivi -Schio,Veneto,Italia,8 Februari1947) alikuwamtumwa kutokaDarfur, wakabila laWadaju[2][3] nchiniSudan ambaye kisha kuletwa Italia akawa huru,akabatizwa, akajiunga nashirika laWakanosa, akaishi na kufanya kazi huko kwa miaka 45[4].
Papa Yohane Paulo II alimtangazamwenye heri tarehe17 Mei1992 namtakatifu tarehe1 Oktoba2000.
Katikafamilia yake aliishi kwafuraha[6] pamoja nandugu zake sita (watatuwa kiume na watatuwa kike) hadi alipotekwa naWaarabu waliofanyabiashara ya utumwa akiwa naumri wa miaka 7/9, mnamoFebruari1877, kama ilivyomtokeadada yake miaka miwili ya nyuma.
Baada ya kulazimishwa kusafiri miguu mitupukilometer 960 (mi 600) hadiEl Obeid; njiani aliuzwa na kununuliwa mara mbili tayari. Katika miaka 12 iliyofuata (1877–1889) aliuzwa tena mara tatu.
Inasemekana kwambauchungu wa matukio hayo ulimfanya asahaujina lake, akaanza kutumia lile alilopewa na mabwana wake,Bakhita, kwaKiarabuMwenyebahati.[7][8]
Piaalisilimishwa.[9]
Huko El Obeid, Bakhita alinunuliwa na Mwarabutajiri sana aliyemtumia kuhudumia mabinti wake wawili waliompenda na kumtendea vema. Lakinikaka yao alimpiga kikatili hivi kwamba alishinda kusimama tena zaidi ya mwezi mzima.
Baadaye alinunuliwa najeneraliMturuki ili kuhudumiamama mkwe namke wake ambao wote walikuwa wakatili kwa watumwa. Bakhita alisema: "Katika miaka mitatu niliyokaa katika nyumba hiyo, sikumbuki siku iliyopita bila majeraha ya viboko. Jeraha lilipotaka kupona, viboko vingine vilinipata.[10]
Pia alisema kuwa kumbukumbu ya kutisha zaidi ya wakati ule ni ile ya kuchanjwa (kama watumwa wengine) kwa ukatili mkubwa kifuani, tumboni na mkononi.[11][12][13]
Mwishoni mwa mwaka1882, El Obeid ilitaka kushambuliwa wa askari waDola la Mahdi,[14] hivyo jenerali aliuza watumwa wake wote isipokuwa 10 aliokwenda kuwauzaKhartoum.
Huko mwaka1883 Bakhita alinunuliwa nabalozi mdogo wa Italia, Callisto Legnani, aliyekuwa mwema sana, hivyo hatimaye Bakhita aliweza kutulia.
Karibu miaka miwili baadaye, Legnani alipotakiwa kurudi Italia, Bakhita alimuomba aende naye. Mwishoni mwa mwaka1884 walifaulu kukimbia Khartoum iliyozingirwa wakiwa na rafiki yao, Augusto Michieli. Kisha kusafiri katika hatari kubwa kilometa 650 (maili 400) wamepandangamia hadiSuakin,bandari kuu ya Sudan.
Mnamo Machi1885 waliondoka Suakin wakafikia bandari yaGenova, Italia mnamo Aprili. Huko Callisto Legnani alimtoa Bakhita kwa Turina Michieli, mke wa Augusto, kama "zawadi".
Mabwana wapya wa Bakhita walikwenda naye Zianigo, karibuMirano Veneto, kilometa 25 (maili 16)magharibi kwaVenice.[11] Huko aliishi miaka mitatu akawayaya wa Alice Michieli, ambaye aliitwa piaMimmina, na aliyezaliwa mnamo Februari1886.
Tarehe29 Novemba1888, Turina Michieli aliwaacha Bakhita na Alice kwamasista Wakanosa huko Venice ili amfuatemumewe Sudan. Aliporudi kuwachukua aende nao Suakin, Bakhita alikataa katakata, ingawa bibi Turina alimshinikiza siku tatu mfululizo.
Kesi ilipopelekwamahakamani, tarehe 29 November1889 uamuzi ukawa kwamba Bakhita hajawahi kuwa mtumwa kisheria, kwa sababu huko Sudan utumwa ulikatazwa kabla hajazaliwa, tena Italia hakuna kabisa.
Hivyo kwa mara ya kwanza Bakhita alijikuta ana maamuzi yote juu ya maisha yake. Akachagua kubaki na Wakanosa.[15]
Tarehe9 Januari1890 Bakhita alibatizwa kwa jina la Yosefina MargaretFortunata (ndiyo tafsiri yaBakhita). Siku hiyohiyo alipatakipaimara na kupokeaekaristi kwa mikono yakardinali Giuseppe Sarto, ambaye baadaye akawaPapa Pius X akatangazwamtakatifu.[16]
Tarehe7 Desemba1893 Bakhita aliingiaunovisi na tarehe8 Desemba1896 aliwekanadhiri zake.
Mwaka1902 alipangwa kwenyekonventi yaSchio,Vicenza, alipoishi miaka yote hadi kifo chake, isipokuwa miaka1935-1939 alipoishiVimercate (Milan pamoja na kutembelea jumuia nyingine za Wakanosa ili kutimiza agizo la kushirikisha mang'amuzi yake na kuandaa masista vijana kwendaAfrika kamawamisionari.[16] Inasemekana "akili yake ilikuwa daima kwa Mungu, na moyo wake huko Afrika".[17]
Huko Schio, Bakhita alifanya kazi kamampishi,mtunzasakristia nabawabu. Hasa katika kazi hiyo alikuja kujulikana na wenyeji kwaupole,utulivu natabasamu yake.Kitabu cha kwanza juu yake (Storia Meravigliosa, kazi ya Ida Zanolini) mwaka1931 kilimfanya ajulikane na wengi nchini kote.[2][18]
Wakati waVita vikuu vya pili (1939–1945) wakazi wa Schio walitegemea ulinzi wake, na kweli mabomu mengi yaliyorushwa kijijini hayakuua mtu yeyote.
Miaka ya mwisho alisumbuliwa na maradhi na maumivu mengi, akitumia baiskeli ya magurudumu matatu, lakini hakupotewa na tabasamu yake. Alipoulizwa anajisikiaje, jibu lilikuwa, "Bwana anavyotaka".
Saa za mwisho akili yake ilirudia mateso ya utumwani akalia, "Minyororo inanibana mno, muilegeze kidogo, tafadhali!". Alipozinduka, aliulizwa: "U hali gani? Leo niJumamosi". "Ndiyo, nina furaha iliyoje: Bibi yetu... Bibi yetu!". Ndiyo maneno yake ya mwisho.[19]
Bakhita alifariki saa 2:10usiku tarehe 8 February 1947. Siku tatu mfululizo watu waliandamana kuheshimu masalia yake kabla hajazikwa.
Alipoulizwa namwanafunzi: "Kama ungekutana na waliokuteka, ungefanya nini?", akajibu bila kusita: "Kama ningekutana na walioniteka, na hata walionitesa, ningepiga magoti na kubusu mikono yao. Kwa sababu, kama mambo hayo yasingetokea, leo singekuwa Mkristo wala mtawa."[20][21][9][22]
Papa Benedikto XVI, mwanzoni mwa hati "Spe Salvi" ("Tumeokolewa katika tumaini") ya tarehe30 Novemba2007, alisimulia kifupi maisha yake kama kielelezo chatumaini la Kikristo.[23]
Bakhita: From Slave to Saint(2009)
| Makala hii bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuiongezea habari. |