Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Yongle

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kaisari Yongle
Ramani ya maeneo yaliyotawaliwa na Yongle ("Ming Empire" mnamo mwaka 1409)
Sanamu ya shaba ya Kaisari Yongle. Hii ni nakala ya sanamu asilia ya jiwe ambayo iliharibiwa wakati waMapinduzi ya Kitamaduni

Kaisari Yongle (tamka: yong-luh;2 Mei1360 -12 Agosti1424) - jina la binafsiZhu Di (WG:Chu Ti) - alikuwakaisari wa tatu wanasaba ya Ming, aliyetawala kuanziamwaka1402 hadi 1424.

Zhu Di alikuwamtoto wa nne wa KaisariHongwu aliyeanzishanasaba yaMing .Cheo chake cha kwanza kilikuwa Mwanamfalme wa Yan akipewautawala juu ya eneo laBeijing kaskazini mwaufalme wa Ming mnamoMei1370. Huko alipaswa kupigana dhidi yaWamongolia wanasaba ya Yuan yaKaskazini. Katika mapigano hayo Zhu Di aliweza kuwekamsingi wajeshi lake la binafsi.Baba yake alipomteuampwa wake Zhu Yunwen kama mfalme mteule alikubali mwanzoni. Lakini baada ya Zhu Yunwen kushika utawala kwa jina laJianwen na kuanza kuwauawajomba wake, Zhu Di aliamua kuasi dhidi ya mpwa wake. Mnamo1402, alifanikiwa kupindua mpwa wake na kutekamji mkuu wa ufalmeNanjing. Hapo alitangazwa Kaisari akachukua jina la Yongle, inayomaanisha "furaha ya milele".

Ili kuimarisha utawala wake na kukazia uhalali wake mwenyewe, Zhu Di alijaribu kufutakumbukumbu ya enzi ya KaisariJianwen akaamuru kuteketeza au kubadilishataarifa nahati zilizohusu utoto na uasi wake. Alifukuzawataalamu wengi waliowahi kuhudumiaserikali huko Nanjing akatoamamlaka kubwa kwapolisi wa siri.[1] Kati ya watumishi wapya waliopanda sasa ngazi chini yake alikuwaZheng He, aliyeendelea baadaye kuzinduasafari kubwa zaupelelezi katikaBahari ya Pasifiki Kusini naBahari Hindi hadiAfrika ya Mashariki.

Kaisari aliamua pia kuhamisha mji mkuu kurudi tenaBeijing.

Aliagiza kufanya matengenezo kwenye Mfereji Mkubwa wa China ulioendelea kuinuauchumi wahimaya yake. Beijing alielekezaujenzi waMji Haramu.

Kwa kusudi la kuimarisha utawala wake alipanua mfumo wa mitihani ambako kila mgombea kwa huduma yaserikali alipaswa kupita.

Aliagiza pia kutungwa kwaKamusi Elezo ya Yongle (Yongle Encyclopedia) iliyokuwakamusi elezo kubwaduniani hadi mwaka2007 ilipopitiwa naWikipedia.

Kaisari Yongle aliagadunia wakati alipoongoza mapigano ya kijeshi dhidi ya Wamongolia. Alizikwa kwenyekaburi la Changling, ambalo ni kaburi la kifalme kubwa zaidi kati ya makaburi ya Ming yaliyopo upande wa kaskazini mwa Beijing.

Marejeo

[hariri |hariri chanzo]
  1. Crawford, Robert B. "Eunuch Power in the Ming Dynasty".T'oung Pao, 2d Series, Vol. 49, Livr. 3 (1961), pp. 115–148. Accessed 9 Oct 2012.

Viungo vya Nje

[hariri |hariri chanzo]
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Yongle&oldid=1102791"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp