Yesu (kwaKiebrania יֵשׁוּעַ, Yeshua,kifupisho cha יהושע, Yehoshua, yaani "Mungu anaokoa") alikuwaMyahudimwanamume aliyeishi miaka 2000 hivi iliyopita (labda6 KK -30BK).
Alizaliwa nabikira Maria kwa uwezo waRoho Mtakatifu, hukoBethlehemu yaUyahudi.Maisha yake yalikuwa ya pekee kwa kuwa alifahamu vitu vingi kwa mfano: sheria hata kuwazidi walimu wa sheria japokuwa hakusomea sheria. Alifanya pia maajabu mengi.
Papyrus P52, iliyoandikwa kwaKigiriki mwaka125 hivi, inahesabika kuwa andiko la zamani zaidi kutufikia kuhusu Yesu. Ina sehemu zaInjili ya Yohane; mbele 18:31-33, nyuma 18;37-38.
Nje yaUkristo kuna habari fupi kuhusu Yesu katika maandiko yawaandishi waRoma,Wagiriki na Wayahudi. Habari hizo zinaangaliwa sana kwa sababu zimetungwa na watu wasiomwamini Yesukidini. Kwa ujumla zinathibitisha ya kwamba Yesu alikuwepo, na kwamba wakati hao walipoandika alikuwa nawafuasi hukoRoma na ya kwamba awali Waroma hawakuelewa tofauti kati ya wafuasi wake na Wayahudi.
2. Mwandishi MromaTacitus: huyo aliandika mnamo mwaka117 ya kwambaKaisari Nero alishtaki kikundi cha “Chrestiani” ya kuwa wamechomamotomji wa Roma. Aliongeza: “Mtu ambaye ni asili ya jina hilo ni Chrestus aliyeuawa wakati waTiberio kwaamri yaPontio Pilato” (Annales XV,44).
3. Mwandishi MromaSvetonius: huyo alimtaja “Chrestos” katika kitabu chake juu yamaisha yaKaisari Klaudio (25,4) ya kwamba huyu amesababishafujo kati ya Wayahudi wa Roma hivyoKaisari aliwafukuza wote mjini.
Vilevile maliwali wa Kirumi waliowekwa pengine kutawala nchi au sehemu fulani walionyesha mara nyingi ukatili nadharau kwa Waisraeli na dini yao, hata kusababishachuki na mapigano kati yajeshi na wananchi. Mfano mmojawapo niPonsyo Pilato aliyesimamiaUyahudi kuanzia mwaka26 hadi36 BK.
Lugha hiyo ndiyo iliyotumiwa na waandishi wote wa Agano Jipya ili vitabu vyao viwafaidishe watu wengi zaidi, ingawa baadhi yao hawakuijua vizuri.
Lugha mama ya Yesu na ya Mitume ilikuwaKiaramu ambacho ni jamii yaKiyahudi na ambacho polepole kilishika nafasi yake kati ya Wayahudi kuanziakarne ya 6 KK.
Hao wote walitokeamkoa waGalilaya, uliokuwa na mchanganyiko wa watu (Waisraeli na mataifa), kiasi kwamba huko Wayahudi wenyewe walifuata kwa urahisidesturi za Kiyunani hata wakadharauliwa na wenzao waKusini (Yerusalemu na mkoa waYudea).
Kati ya mikoa hiyo miwili ulienea mkoa waSamaria ambao wakazi wake walijengauadui mkubwa na Wayahudi baada yauhamisho wa Babeli, walipokataliwa kuchangiaujenzi wahekalu la pili la Yerusalemu.
Dionisi Mdogo,mmonaki aliyeanzisha (mwaka533 hivi) mtindo wa kuhesabu miaka tangu kuzaliwa Yesu kurudi nyuma (K.K.) au kwenda mbele (B.K.), alikoseahesabu zake. Leo tunakisia Yesu alizaliwa mwaka 6 hivi K.K. kwa sababu alizaliwaBethlehemu chini ya Herode Mkuu aliyefariki tayari mwaka 4 K.K.
Huyo alipojaribu kumuuamtoto Yesu,familia takatifu ilikimbiliaMisri mpaka baada ya kufa kwa Herode. Hapo ikarudi Galilaya hata Yesu akajulikana kwa jina lakijiji chaNazareti kilichodharauliwa na Wagalilaya pia. Ndipo alipokulia na kuishi akifanyakazi yaufundi.
Hivyo Yesu alitumia sehemu kubwa ya maisha yake kijijini akiwatii wazee wake Maria na Yosefu na kufanya kazi zamikono. “Alishuka pamoja nao mpaka Nazareti, naye alikuwa akiwatii” (Lk 2:51). Kwa namna hiyo ametuachia kielelezo chautakatifu katikamaisha yafamilia na ya kazi ambayo ndiyo njia ya kawaida ya kukomaa kiutu na kumtumikia Mungu. “Mnyenyekeane katika kicho cha Kristo” (Ef 5:21).
Ingawa huyo akamfunga mapema akamuua, kazi ya Yohane ilikuwa imetimia kwa sababu aliweza kuwaandaa Waisraeli wengi (hasa watu wadogo nawakosefu) wampokee Yesu aliyebatizwa naye. Katika nafasi hiyo Yohane alimtambulisha kamaMwanakondoo wa Mungu aondoayedhambi yaulimwengu.
Ndipo Yesu naye alipoanza kuhubiri, lakini pia kutendamiujiza ya kila aina, akapata haraka wafuasi wengi. Kati yao akachaguaMitume wake 12 kamamsingi mpya wataifa la Mungu badala ya Israeli ya kale.
Alifanya kazi hizo kuanzia Galilaya, akitangazaujio waufalme wa Mungu, kwa maana ya kwambaufalme uliotazamiwa na Wayahudi umewajia kwa njia yake.
Mafundisho yake yalilingana na yale yaMafarisayo kuliko na yale yaMasadukayo, lakini alishindana pia na hao wa kwanza.
Kijicho naupinzani vikazidi hasa Yerusalemu, walipoanza kufanyanjama za kumuua. Ingawa Yesu alijua hayo, alijikaza kwenda katika huomji mtakatifu autangazie habari njema na kufia huko.
Hata hivyosiku yatatu kaburi likaonekana tupu, na Yesu akaanza kuwatokea wanafunzi wakewa kike na wa kiume kwa muda wasikuarubaini, halafuakapaa mbinguni mbele ya macho yao.
Habari hizo zikatangazwa kwasauti tu kwa miaka kadhaa, halafu zikaanza kuandikwa.
Kanisa linaheshimu kwa namna ya pekee, kamaushuhuda mkuu juu ya maisha na mafundisho ya Yesu na kamamoyo wa Maandiko matakatifu yote, Injili nne zilizoandikwa naMarko,Mathayo,Mwinjili Luka naYohane kati ya mwaka65 na100 hivi.
Ni muhimu kujua maisha ya Yesu kwa sababu matendo na maneno yake, pamoja nakimya nasala yake, na hasakifo naufufuko wake, yote yanatufunuliaBaba na matakwa yake kwetu. “Mambo ya Yesu wa Nazareti, aliyekuwa mtu nabii, mwenye uwezo katika kutenda na kunena mbele za Mungu na watu wote” (Lk 24:19).
Baada ya kujua maisha ya Yesu tunapaswa kujilinganisha naye hadi aundwe na kuishi ndani mwetu akitushirikishauhai, kifo na ufufuko wake. “Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu, na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu… Vitoto vyangu, ambao kwamba nawaonea utungu tena mpaka Kristo aumbike ndani yenu!” (Gal 2:20; 4:19).
Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi,kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili,ukawafunulia watoto wachanga.Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako
(Yoh 11:41-42)
Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia.Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote;lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya,ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma.
(Yoh 17:1-26)
Baba, saa imekwisha kufika.Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako naye akutukuze wewe;kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote wenye mwili,ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele.Na uzima wa milele ndio huu:wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma. Mimi nimekutukuza duniani, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye.Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja nawe,kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako. Jina lako nimewadhihirishia watu wale ulionipa katika ulimwengu; walikuwa wako, ukanipa mimi, na neno lako wamelishika.Sasa wamejua ya kuwa yote uliyonipa yatoka kwako.Kwa kuwa maneno uliyonipa nimewapa wao;nao wakayapokea, wakajua hakika ya kuwa nalitoka kwako,wakasadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.Mimi nawaombea hao; siuombei ulimwengu;bali hao ulionipa, kwa kuwa hao ni wako;na wote walio wangu ni wako, na walio wako ni wangu;nami nimetukuzwa ndani yao.Wala mimi simo tena ulimwenguni,lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako.Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa,ili wawe na umoja kama sisi tulivyo.Nilipokuwapo pamoja nao,mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza;wala hapana mmojawapo wao aliyepotea,ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie.Na sasa naja kwako;na maneno haya nayasema ulimwenguni,ili wawe na furaha yangu imetimizwa ndani yao.Mimi nimewapa neno lako, na ulimwengu umewachukia,kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu;bali uwalinde na yule mwovu.Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli.Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni,nami vivyo hivyo naliwatuma hao ulimwenguni.Na kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe,ili na hao watakaswe katika kweli.Wala si hao tu ninaowaombea;lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao.Wote wawe na umoja;kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako,hao nao wawe ndani yetu,ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao,ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja.Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma,ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi.Baba, hao ulionipa nataka wawe pamoja nami popote nilipo,wapate na kuutazama utukufu wangu ulionipa;kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa msingi ulimwengu.Baba mwenye haki, ulimwengu haukukujua;lakini mimi nalikujua, na hao wamejua ya kuwa ndiwe uliyenituma.Nami naliwajulisha jina lako, tena nitawajulisha hilo,ili pendo lile ulilonipenda mimi liwe ndani yao, nami niwe ndani yao.
(Mk 14:36)
Aba, Baba, yote yawezekana kwako; uniondolee kikombe hiki;walakini, si kama nitakavyo mimi, bali utakavyo wewe.
(Mk 15:34)
Eloi, Eloi, lama sabakthani?(maana yake, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?)
Waumini wake wanaunda Kanisa la Kikristo ambalo linapatikana leo katikamadhehebu mengi. Karibu wote wanamwamini kuwa Mungu aliyechukuaumbile la mwanadamu au, kwa lugha nyingine, kuwaMwana wa Mungu.
Kwa imani hiyo, Yesu ni Mungu na mtu kwa pamoja, ndiyo sababu ni mshenga pekee kati ya Mungu na watu. “Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, mwanadamu Kristo Yesu” (1Tim 2:5). “Katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili” (Kol 2:9). Hivyo ni Mungu kweli na mtu kweli.
Umungu na utu wa Yesu vimeunganika katika nafsi moja visichanganyikane, kwa kuwa ndani yake hali hizo mbili zinatenda kila moja ya kwake. “Basi yule akida, aliyesimama hapo akimwelekea, alipoona ya kuwa alikata roho jinsi hii, akasema, ‘Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu’” (Mk 15:39).
Mwana wa Mungu tanguatwae mwili ni mtu kamili mwenye akili na utashi wa kibinadamu. Katika umoja wa nafsi yake vipawa hivyo vinatenda kulingana na Umungu anaouchanga na Baba na Roho Mtakatifu milele. “Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake” (Yoh 14:10).
Hapaduniani Yesu alizaliwa naBikira Maria kama malaika alivyomuambia: “Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo, hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu” (Lk 1:35).
Hata hivyo Wakristo wachache wanaamini kuwa yeye nimtume wa pekee wa Mungu ila si Mungu.
Katika dini yaUislamu, Yesu anajulikana kamaNabiiIsa. Waislamu wanaamini kuwa yeye alikuwa nabii wa Mungu ila hakuwa mwana wa Mungu wala Mungu.
Maisha yake yamekuwa msingi wasikukuu mbalimbali zinazosheherekewa katika nchi nyingi duniani, kama vile Noeli auKrismasi (kuzaliwa kwake),Epifania (kuonekana kwake na kubatizwa kwake),Majilio (kuandaliwa kwa ujio wake wa kwanza na kutarajiaujio wa pili),Kwaresima (mafungo namateso yake),Ijumaa Kuu (kifo chake); muhimu kuliko zote niPasaka (kufufuka kwake).
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuYesu kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.