Mto Yangtze, ambayo ni mto mrefu Asia na huesabika kama mto watatu mkubwa dunia nzimaPinde la kwanza la Yangtze katika jimbo laYunnan ambako mto hugeukia 180° kutoka mwelekeo wa kusini kuelekea kaskazini
Mto Yangtze (pia:Changjiang) ni mto mkubwa nchiniChina na pia mto mrefu waAsia yote. Duniani huhesabiwa kama mto mrefu wa tatu baada yaAmazonas naNaili).
Mwendo wake wote wa kilomita 6,300 pamoja na kilomita 2,800 zinazotumiwa na meli uko ndani ya China.
Chanzo chake iko katika nyanda za juu za Tibet. Inafuata mwelekeo wa kusini-mashariki hadi kilomita 1,500 baada ya chanzo. Hapa inasimamishwa na milima yenye mawe magumu na kugeuka ikuelekea sasa kwenda kaskazini-mashariki.
Katikati ya mwendo wake mto hupita kwenye mabode makali. Hapa serikali ya China iliamua kujengalambo la magenge matatu linalo umbara zake zimeonakana kwa sababu watu milioni 1.5 walipaswa kuhamishwa na tayari tatizo la matope kujaza ziwa nyuma ya lambo limeshaanza.
Kuna miji mingi mikubwa inayotegemea mto huu na machafuko kutoka ya viwanda vyao yamekuwa tatizo.
Katika historia mwendo wa Yangtze ilikuwa mpaka kati ya China ya kaskazini na China ya kusini.
Makala hii kuhusu maeneo yaChina bado nimbegu. Je unajua kitu kuhusuYangtze (mto) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.