Y ni herufi ya 25 katikaalfabeti ya Kilatini ambayo ni pia mwandiko waKiswahili cha kisasa. Asili yake niIpsiloni yaalfabeti ya Kigiriki.
Historia ya Y ina asili za pamoja na U, W, V na F. Historia hii ni ngumu kidogo kwa sababu alama ilipita katika alfabeti za lugha ambazo zilitumia hasa alama hii kwa sauti tofautitofauti. Kwa sababu hii matamshi yalibadilika kati ya lugha na lugha. Pia lugha mpya iliweza kuona haja ya kuunda alama mpya kwa sauti ya pekee.
Alama ya Y kiasili haikupatikana katika Kilatini cha Kale. Ilihitajika baada ya Roma kutawala Ugiriki na lugha ya Kilatini kupokea maneno mengi ya Kigiriki yaliyokuwa na herufi yaipsiloni.
Asili yake ni "waw" yaKifinisia iliyokuwa kiasili picha iliyorahisishwa ya fimbo la kingoe au kiopoo. Wagiriki wa Kale walichukua alama hiyo na kuitumia kwa namna mbili: kwa umbo moja kamadigamma (tazamaF) na umbo la pili kama "ipsilon" bila kujali maana asilia ilitaja sauti kati ya "u" na "i".
Ipsiloni iliingia tayari mwanzoni katika alfabeti ya Kilatini kupitiaKietruski lakini kwa sauti ya "u/v". Kwa hiyo iliigizwa mara ya pili kwa maana yake ya Kigiriki.
Katika lugha kadhaa inaonyesha leokonsonanti (kamaKiswahili) katia lugha kadhaa huonyeshavokali kama "i" yaKijerumani /Kituruki "ü". KatikaKiingereza ni mara konsonanti mara vokali.