Xi'an (Sian) 西安市 Nchi China Jimbo / Mkoa Shaanxi Anwani ya kijiografia 34°15′54″N 108°57′14″E Kimo m 405 Eneo km2 1,088 Wakazi 7,135,000[ 1] Msongamano wa watu 6,600/km2 Simu 29 Tovuti rasmi www.xa.gov.cn
Mahali pa Xi'an katika China Xi'an nimakao makuu yaMkoa waShaanxi nchiniChina . Kwenyemwaka 2011 ilikuwa na wakazimilioni 6.[ 2]
Jiji hilo ni maarufu kwaJeshi la Matofali lililopatikana ndani yakaburi lakaisari wa kwanza waChina Qin Shi Huang .[ 3]
Mji huu ulikuwamji mkuu wanasaba za wafalme 13, pamoja nanasaba yaZhou ,nasaba yaQin ,nasaba yaHan ,nasaba yaSui , nanasaba yaTang .
Umuhimu wa mji ulitokana na mahali pake kwenye chanzo chaBarabara ya Hariri iliyounganisha China naAsia ya Magharibi naya Kusini [ 4] .
Xi'an inachukuliwa kuwa moja ya taji za kongwe zaidi katikahistoria yaulimwengu pamoja na nyingine tatu zaAthene ,Roma naCairo .
Xi'an ilijulikana zaidi kwatahajia ya Sian. Jina la Xi'an lilichaguliwa kwa maana ya "Amani ya Magharibi" wakati wanasaba yaMing kwa sababu ilikuwa mji mkubwa kwenye magharibi yamilki ya Ming .
Kama mji wa kihistoria, Xi'an bado imezungukwa naukuta wa kale. Kivutio kikuu cha wageni ni makaburi ya kifalme pamoja na "jeshi la matofali". Halafu: