Picha ya Xerxes kwenye mwamba wa nguzo huko Persepolis
Xerxes I alikuwaShah (mfalme) waUajemi ya Kale kuanzia 485 KK hadi 465 KK. Alikuwa mtawala wa 10 katikanasaba ya Waakhameni. Xerxes alikuwa mwana waDario I na Atossa, binti yaKoreshi Mkuu . Baada ya kifo cha Dario, Xerxes akawaShah waUajemi . Alichukua cheo chaShahanshah (Mfalme wa Wafalme ).
Xerxes (Ξέρξης) ni umbo laKigiriki la jina lake. Kwa Kiajemi ya Kale lilikuwaXšaya-ṛšā. Mataifa mengine katika ufalme wake yalitafsiri jina hili kwa namna tofauti Inaaminiwa umbo laKibabeliAkšiwaršu lilipokelewa katikaKiebrania kamaAhasverus[1].
Xerxes alikuwa mfalme wakati baba yake Dareio alikuwa akiandaa vita dhidi ya Ugiriki baada ya kupigwa na Waathens katikaMapigano ya Marathon. Alikusanya jeshi kubwa kutoka pande zote za milki yake akavukamlangobahari wa Dardaneli kwa kujenga daraja. KatikaMapigano ya Thermopylae, Xerxes alishinda kikosi cha jeshi laSparta na kuteka sehemu zaUgiriki . Baada ya ushindi huko Thermopylae, Xerxes alivamia pia mji waAthens akaichoma. Lakini watu wa Athens waliwahi kujiokoa kwenye kisiwa cha Salamia. Manowari za Wagiriki zilishambulia Waajemi katikamapigano ya baharini ya Salamis mnamo mwaka480 KK zikashinda. Xerxes aliamua kurudi upande wa Asia akiacha jeshi katika Ugiriki lakini pia jeshi hilo lilipigwa na wagiriki katika mapigano ya Plataia mwaka 479 KK[2].
Baada ya vita ya Ugiriki, Xerxes alirudi Uajemi akashughulika kukamilisha miradi ya ujenzi iliyoanzishwa na baba yake Dareio I hasa katika miji mikuu yaShushani naPersepolis. Mapambo mengi yanayoonekana huko Persepolis hadi leo yaliumbwa wakati wa Xerxes. Huko Shuhani alitengeneza ikulu kubwa.
Alitengeneza pia barabara ya kifalme kutoka Shushani hadi Sardis katikaAsia Ndogo.
KatikaKitabu cha Esta chaBiblia kuna simulizi ya binti Myahudi Esta anayeolewa na mfalme wa Uajemi anayeitwa Ahasuero katika tafsiri ya Kiswahili (Kiebrania אֲחַשְׁוֵרֹ֑ושׁAhasverus) . Kitabu hiki kinasimulia habari zilizotokea katika mji mkuu Shushani. Ahasuero ni umbo tofauti la "Xerxes", maana wafalme wote waliotawala milki ya mataifa mengi walijulikana kwa majina tofautitofauti.
↑https://iranicaonline.org/articles/ahasureus W. S. McCullough, “AHASUREUS,” Encyclopædia Iranica, I/6, pp. 634-635; online hapa http://www.iranicaonline.org/articles/ahasureus (accessed on 16 March 2014).