Asili yake nimvuke wa maji unaotokea wakatijua linabadilisha maji kuwagesi ya H²O;mvuke unapanda juu kwa sababu ni nyepesi kulikohewa. Baada ya kupanda kiasi cha kutosha hufikia umbali penye baridi na mvuke unatonesha kuwa matone madogo ya maji. Kama wingu ni juu sana baridi inasababisha mvuke kuwafuwele zabarafu autheluji.
Mvuke unahitaji viini kwa kutonesha. Viini hivi ni aina zote za vumbi iliyoko hewani. Mvuke uliopo hewani unaanza kutonesha kwenye vipande hivi vidogo sawa na mvuke katika chumba cha jikoni au bafuni unaotonesha kwenye kioo cha dirisha au ukutani.
Matone ndani ya wingu yanaweza kueleaangani kwa muda mrefu kama ni madogo. Mara nyingi matone madogo huwa na kipenyo chamilimita 0.001 hadi 0.015 hivyo ni nyepesi na mwendo wa kuanguka ni polepole. Hali halisi hayaanguki kwa sababu mawingu hutokea sehemu penye upepo wa kupanda juu na mwendo wa upepo huzidi au kulingana na mwendo wa kuanguka kutokana nagraviti.
Lakini matone yana mwelekeo wa kuungana na kuwa makubwa zaidi. Yanaweza kufikia kipenyo cha milimita 1-3 na kuwa mazito zaidi. Sasa uvutano wa graviti unapita mwendo wa upepo na matone yanaanza kuanguka chini kamausimbishaji.