Wilaya ya Marakwet ilikuwawilaya mojawapo yaMkoa wa Bonde la Ufa waJamhuri yaKenya hadi ilipopitishwakatiba mpya ya nchi (2010).
Makao makuu yalikuwamjiniKapsowar.
Kwa sasa imekuwa sehemu yakaunti ya Elgeyo-Marakwet.
Wilaya hii ilikuwa na jumla ya wakazi 140,629[1]. Wakaazi wenyeji ni haswa wa kabila laWamarakwet.
Wilaya hii iliundwa mwaka wa 1927 kamaElgeyo/Marakwet District. Iligawanywa mara mbili na kuundaWilaya ya Keiyo na Marakwet mwaka wa1994.
Wakimbiaji wengi mashuhuri Wakenya hutoka Marakwet, na wanaojulikana ni pamoja naMoses Kiptanui,Evans Rutto,Reuben Kosgei,Ezekiel Kemboi naRichard Chelimo.
Wilaya hii ilikuwa na serikali ya mtaa moja tu, Baraza la Mji wa Marakwet. Kwa hiyo, idadi yake ya watu ni sawa na idadi ya wilaya (140,629). Baraza na Wilaya haina idadi ya wakaazi wanaotambulika kama wakaazi wa mjini (sensa ya 1999)[2].
Tarafa | Idadi ya Watu | Makao makuu |
---|---|---|
Chebiemit | 18,559 | Chebiemit |
Kapcherop | 39,328 | Kapsowar |
Kapsowar | 19,647 | Kapsowar |
Kapyego | 11,452 | Kapyego |
Tirap | 23,311 | Kapchebau |
Tot | 17,744 | Tot |
Tunyo | 10,588 |
Eneo la wilaya hii lina maeneo bunge mawili: