Mada ambazo zinakosekana kwa Kiswahili kulingana na orodha ya makala 1000 za msingi
Mnamo Februari 2021 zimebaki mada 3 za orodha ya makala 1000 za msingi katika Wikipedia ya Kiingereza (ambayo ni Wikipedia kubwa zaidi, hivyo ni ya msingi kwa kazi hii yote) ambazo hazijaonekana katika Wikipedia ya Kiswahili. Upande wa kushoto (buluu) unaonyesha makala za Kiingereza, upande wa kulia (nyekundu) ni viungo vya Wikipedia ya Kiswahili ambavyo makala hizo haziko bado:
- conservation of energy - sw:hifadhi ya nishati
- general relativity - sw:uhusianifu majumui ?
- infinity - sw:msopeo? -bila kikomo ?
Chanzo chake niMakala zisizoonekana kati ya 1000 za msingi - Absent_Articles#sw_Kiswahili. Ila wakati mwingine roboti zinazolinganisha Wikipedia mbalimbali zinaweza kukosea. Kwa mfano hazikutambua makala ya _Brussels_ katika Wikipedia yetu na kuiandika katika orodha hii - kumbe makala ipo. Yeyote anayetambua kosa la aina hii anaweza kuisahihisha kwa kuingiza kwa mkono makala husika ya Wikipedia ya Kiswahili.
Kwa orodha kamili ya makala zote 1000 tazama hapa:Wikipedia:Makala za msingi za kamusi elezo/Zote 1000.
Kila mwanawikipedia anaombwa
- kuanzisha kwa Kiswahili au kutafsiri makala hizo tatu. Kubofya jina jekundu upande wa kulia kutaanzisha makala mpya kwa Kiswahili. Kama ni jina la Kiingereza bado, ulitafsiri kabla ya kuanza.
- Kuboresha michango mingine iliyopo katika orodha ya "makala 1000" kwa kuiongezea matini maana kurasa nyingine bado ni fupi sana.