Wasuni nidhehebu kubwa ndani ya dini yaUislamu. Takriban asilimia 80 - 90 za Waislamu wote duniani hukadiriwa kuwa Wasuni na wengine 10-20 % huhesabiwa kati yaWashia.
Wasuni huitwa kwa Kiarabuahl ul-sunna (Kiarabu:أهل السنة; "watu wa mapokeo"). Neno Suni hutokana na nenosunna (kwa Kiarabu :سنة ) inayomaanishamapokeo yaMtume Muhammad.
Wasuni hufuata mwelekeo wa Uislamu ulioanzishwa na ukhalifa waAbu Bakr na kutokubali uongozi wa familia ya Mtume Muhammad kupitiaAli,Hassan naHusain.
Madhehebu ya Wasuni
Kati ya Wasuni kuna madhehebu nne zinazotofautiana kiasi kuhusu mafundisho yasharia au sheria ya kidini ya Kiislamu. Ndio Wahanafi, Wamaliki, Washafii na Wahanbali. Kwa jumla Wasuni hukubaliana ya kwamba madhehebu haya yote manne ni sawa.
Walimu wengine hasa katika kikundi chaWawahabi kilichoanzishwa kati ya Wahanbali kimekaza mafundisho yake hadi kuwashtaki wengine kuwa si Waislamu wa kweli.