Nguzo ya Washington na Nyumba Nyeupe (White House)
Washington, D.C., rasmi inajulikana kamaWilaya ya Columbia na kwa kawaida huitwaWashington auD.C., ni mji mkuu na wilaya ya shirikisho yaMarekani. Jiji hili liko kwenye Mto Potomac, mkabala naVirginia, na linapakana naMaryland upande wa kaskazini na mashariki. Lilipewa jina laGeorge Washington, rais wa kwanza waMarekani. Wilaya hiyo imepewa jina laColumbia, mfano wa kike wa taifa.
Jina la mji mkuu limechaguliwa kwa heshima ya kiongozi wa uhuru na rais wa kwanzaGeorge Washington. Jina la "District of Colombia" likachaguliwa kwa heshima yaKristoforo Kolumbus mpelelezi wa Amerika.
Washington D.C. ni tofauti najimbo la Washington lililopo upande wa magahribi wa Marekani.
Hapa ni makao rasmi ya Bunge la Marekani, ya Rais pamoja na serikali yake na makao ya mahakama kuu. Kuna pia majengo ya kihistoria hata kama Marekani haina historia ndefu pamoja na makumbusho mazuri.
Makao ya kwanza ya serikali ya Marekani ilikuwa New York. Rais George Washington mwenyewe alichagua eneo la mji mpya kando la mto Potomac mwaka 1790. Ujenzi wa ikulu la Nyumba Nyeupe ulianza 1792. Mpango wa mji ulifuata mfano wa mji waKarlsruhe (Ujerumani).
Hadivita ya wenyewe kwa wenyewe ya Marekani Washington ilikuwa mji mdogo usiozidi wakazi 75,000 lakini ilikua baada ya vita kwa sababu serikali iliongezeka idara na wafanyakazi.
Tangu 1878 mji wa Washington na mkoa wa shirikisho ("D.C.") viliunganishwa. Mji kama mkoa ulitawaliwa moja kwa moja na bunge. Tangu 1973 mji umempata meya na serikali ya kimanisipaa. Kwenye bunge lenyewe hakuna mbunge wa wakazi wa Washington. Kuna mwakilishi wao mle lakini hana kura.
Makala hii kuhusu maeneo yaMarekani bado nimbegu. Je unajua kitu kuhusuWashington, D.C. kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.