Walinzi wa amani wa UM kutoka Nepal nchini Somalia waka 1993
Walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa ni vikosi vyawanajeshi wanaotolewa na nchi wanachama chini ya usimamizi waUM kwa kulindaamani au hali ya kusimamisha mapigano.
Tangumwaka1948 vikosi hivyo vimetumwa kwenda mahali paugomvi katika sehemu mbalimbali zadunia.
Msingi wa kutuma walinzi wa amani ni kibali chaserikali ya nchi husika pande zote katika ugomvi. Vikosi vya walinzi wa amani hawanamamlaka ya kusimama upande mmoja wala kushiriki katika mapigano. Wanatumia silaha kwa ajili ya kujitetea pekee. Hata hivyoBaraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linaweza kutoaamri kwa walinzi wa amani kuendelea kuwalazimisha washiriki katika mapigano. Kwa namna hiyo kikosi maalumu cha UM kilianza kushambuliawanamgambo katikamashariki ya Kongo waliokataa kufuata mapatano ya kusimamisha mapigano na uporaji wa wananchi.
Mwaka2014 kulikuwa na walinzi wa amani mahali 16 duniani wakiwa na jumla ya wanajeshi nawafanyakazi 116.517. Nchi zinazotoa wanajeshi ni hasaPakistan,Uhindi naBangladesh, kila nchi takriban 8.000. Hadi 31 Machi 2014 jumla ya walinzi 3,215 waliuawa, 2320 kati ya hao walikuwa wanajeshi, 232polisi, 322 wafanyakazi wa UM kutoka nchi husika na 228 wafanyakaziraia wa kimataifa.
Walinzi wa amani walifaulu mara kadhaa kutekeleza kusudi lao lakini kuna pia mifano ambapo wameshindwa. Kati ya mifano mibaya iliyoleta upinzani ni Vita ya wenyewe kwa wenyewe nchiniRwanda. HapaBaraza la Usalama la UM ambayo ni bodi pekee kuamulia kuhusu walinzi hao ilisita kupigakura hadimauaji nchini Rwanda yalikuwa na mbio tayari. Mfano mwingine ulikuwaMauaji ya Srebenica nchiniBosnia ambako kikosi cha walinzi wa amani haikuruhusiwa kutumia silaha zake kikapaswa kutazama tu jinsiwanaume raia Wabosnia zaidi ya 8,000 walivyokamatwa na kuchinjwa na wanamgambo waSerbia.