Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Ukoloni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutokaWakoloni)
Ramani ya Ukoloni duniani kabla yaVita ya Miaka Saba mnamo mwaka 1754
Ramani ya ukoloni duniani mwishoni mwaVita Kuu ya Pili ya Dunia mwaka1945.

Ukoloni ni mfumo wataifa moja kuvuka mipaka yake na kutawala maeneo ya mbali yanayokaliwa na watu wengine kwa nyanja zauchumi,utamaduni najamii. Maeneo hayo yanaweza kuitwa makoloni ya kawaida au maeneo lindwa tu.

Jina

[hariri |hariri chanzo]

Neno "koloni" linatokana naKilatinicolonia (kupitiaKiingerezacolony). Ni kwambaRoma ya Kale ilipanua eneo lake kwa kuanzishamiji mipya ya nje kwa kuteuaraia na kuwapaardhi kwa ajili yamashamba huko. Hiyo iliitwa koloni.

Milki nyingine za kale zilitumia mtindo huohuo kama vileWagiriki wa Kale naWafinisia.

Neno hilo la Kilatini lilitumiwa baadaye kwa ajili ya kutaja makazi mapya ya watu kutoka eneo moja katika eneo la mbali. Ilhali hatua hii ilimaanisha mara nyingi pia upanuzi wautawala wa eneo mama, neno likataja baadaye pia eneo linalotawaliwa na nchi ya mbali.

Historia

[hariri |hariri chanzo]

Ukoloni ni hasa ule wa kipindi tangukarne ya 15 ambakoUreno naHispania zilianza kueneza himaya zaoAfrika naAmerika ya Kusini na kudumu pengine hadi baada yaVita Kuu ya Pili ya Dunia.

Lakini kulikuwa na vipindi vya ukoloni pia zamani katikahistoria kama vile ukoloni waRoma ya Kale, ukoloni waWaarabu na wengine. Ukoloni kwa maana hii unaweza kuwa tofauti na kuundwa kwakoloni katika vipindi mbalimbali vya historia ambapo maeneo bila wakazi au yenye wakazi wachache sana yaliingiliwa na watu kutoka sehemu nyingine.

Ukoloni mamboleo ni aina ya nchi au kundi la nchi fulani kutawala nchi nyingine kinyemela kwa kuweka vikwazo na masharti yatakayowafanya watawaliwa waendelee kuwa nauchumi tegemezi ili watajirishe zaidi hao wanaowatawala kinyemela.

Utawala wa kikoloni

[hariri |hariri chanzo]

Utawala wa kikoloni niutawala ulioanzishwa hasa naWazungu kwa lengo lakunyonya na penginekuwabaguaWaafrika na watu wengine wenyeji waAsia,Oseania naAmerika.

Utawala huo ulitegemea hali yataifa husika pamoja na hali yajamii zilizokuwa zinatawaliwa.

Baada ya kuanzisha utawala huo wakoloni walibadilishautawala wa jadi na kuufanya utawale kwamasilahi ya wakoloni; pia utawala huo uliharibuhadhi ya utawala wa jadi na misingi yajadi.

Muundo wa utumishi

[hariri |hariri chanzo]

Muundo wa utumishi katika utawala wa kikoloni ulikuwa wa kibaguzi na kinyonyaji:

(a) Kazi katika ngazi za juu zilifanywa na Wazungu, hasa kazi zilizohitajiujuzi.

(b) Kazi katika ngazi za chini zilifanywa na wenyeji kama vileukarani,utarishi,ufagizi naukorokoroni.

(c) Wakoloni walitoaelimu duni kwa wenyeji ili waendelee kuwaajiri katika ngazi za chini.

Makoloni yaliyokuweko Afrika

[hariri |hariri chanzo]

Nchi zaAfrika ziliwekwa rasmi chini ya ukoloni wa nchi zaUlaya mara baada yaMkutano wa Berlin wa 1885 ulioitishwa nachansella waUjerumaniBismarck mwaka1884-1885.

Nchi zilizojenga ukoloni huo Afrika zilikuwaUingereza,Ufaransa,Ureno,Ujerumani,Uhispania,Italia naUbelgiji.Uholanzikarne za nyuma ilikuwa na Afrika Kusini.

1.Ubelgiji ilikuwa na maeneo yaJamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,Burundi naRwanda ya leo

2.Uingereza ilikuwa naAfrika Kusini,Botswana,Cameroon ya Kiingereza,Gambia,Ghana,Kenya,Lesotho,Malawi,Mauritius,Misri,Nigeria,Shelisheli,Sierra Leone,Somaliland,Sudan,Swaziland,Tanganyika,Uganda,Zanzibar,Zambia,Zimbabwe na sehemu nyingine kwa muda.

3.Ufaransa ilikuwa naAlgeria,Benin,Cameroon,Chad,Cote d'Ivoire,Jamhuri ya Afrika ya Kati,Jibuti,Komoro,Gabon,Guinea,Madagaska,Mali,Mauritania,Moroko,Niger,Senegal,Togo,Tunisia na sehemu nyingine kwa muda.

3.Ujerumani ilikuwa naAfrika ya Kusini-Magharibi ya Kijerumani (leoNamibia),Afrika ya Mashariki ya Kijerumani (tangu 1922Burundi,Rwanda naTanganyika),Kamerun naTogo, lakini baada yavita vikuu vya kwanza ilinyang'anywa kila mojawapo; zilikuwamaeneo ya kudhaminiwa kwa niaba yaShirikisho la Mataifa na kuweka chini ya Uingereza, Ufaransa, Ubelgiji na Afrika Kusini.

4.Italia ilikuwa naEritrea,Libya naSomalia ya Kiitalia; piaEthiopia kwa miaka mitano tu (1936-1941).

5.Ureno ilikuwa naAngola,Cape Verde,Guinea-Bissau,Msumbiji,Sao Tome na Principe

6.Hispania ilikuwa naGuinea ya Ikweta, sehemu za Moroko naSahara Magharibi.

Tazama pia

[hariri |hariri chanzo]

Vitabu

[hariri |hariri chanzo]
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Ukoloni&oldid=1053601"
Jamii:
Jamii iliofichwa:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp