Wakazakhi (kwaKikazakhi Қазақ/Qazaq, wingi Қазақтар/Qazaqtar) nitaifa lenye kutumiaKikazakhi, mojawapo yalugha za Kiturki linalopatikana hasa nchiniKazakhstan, lakini pia katikaMongolia,China,Urusi,Uzbekistan naAfghanistan. Vikundi vidogo zaidi vinapatikanaIran naUturuki.
Idadi ya Wakazakhi hukadiriwa kuwa mnamomilioni 20.
Upande wadini walio wengi niWaislamu Wasunni.
Wakazakhi wametokea katikahistoria ya makabila ya Kiturki katikaAsia ya Kati.Jina "Kazakh" linamaanisha "huru, asiyetawaliwa": lilikuwa namna ya kutaja makabila ya Waturki waliopendelea kufuatamila zao na kujitenga mnamo1450 namilki yaWauzbeki.
Maeneo makubwa walipoishi Wakazakhi yalitwaliwa naUrusi kuanziakarne ya 17 kwa hiyo Wakazakhi wengi waliishi katikaMilki ya Urusi na katikakarne ya 20 katikaUmoja wa Kisovyeti.
Baada yamapinduzi ya kikomunisti Wakazakhi walipewa eneo lao la pekee ndani ya mfumo waukomunisti na tangu mwaka1936 eneo hili lilikuwaJamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kikazakhi, moja kati yajamhuri 17 zilizoundaUmoja wa Kisovyeti. Hiyo ilipatauhuru wake tangu kuporomoka kwa ukomunisti mwaka1991.
Leo hii wanaishi
- Kazakhstan 12,212,645 (2018)[1]
- China1,800,000[2]
- Uzbekistan800,000[3]
- Urusi647,732[4]
- Mongolia201,526[5]
- Kyrgyzstan 33,200[6]
- Marekani24,636
- Uturuki10,000
- Iran3,000–15,000