Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Wakapuchini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wakapuchini niwatawaWafransisko waKanisa Katoliki.

Idadi yao inakaribiawanaume 10,000duniani kote, wakiongozwa na nduguRoberto Genuin wa kanda yaVeneto. Nishirika la kiume lanne kwa wingi wa watawa duniani.

Maana ya jina

[hariri |hariri chanzo]

Jina linatokana naneno laKiitalia "cappuccio", lenye maana ya kikofia kilichoshonwa kwenyekanzu yao yarangi yakahawia.

Historia

[hariri |hariri chanzo]

Tawi hilo lilianzishwa naMathayo wa Bascio pamoja naLudoviko wa Fossombrone naRafaeli wa Fossombronemwaka1525, ambao walilenga maisha ya kifukara kuliko yaliyofuatwa naNdugu Wadogo wenzao.

Urekebisho huo, uliojitahidi sana kufuata kikamilifukanuni ya Ndugu Wadogo na mifano yamwanzilishi,Fransisko wa Asizi, ulipata kibali chaPapa Klementi VII mwaka1528.

Baada ya hapo kutokamkoa waMarche shirika likaenea na kuzaamatunda mengi yautakatifu kuanziabradhaFelix wa Cantalice hadipadriPio wa Pietrelcina.

Bernardino wa Asti, aliyeshikauongozi miaka1535-1538, ndiye aliyelipashirika jipya sura ya kiroho ya kudumu, hasa kwa njia ya katiba iliyotungwa mwaka 1535 na kupitishwa mwaka uliofuata, halafu ikatumika hadi mwaka1968 bila mabadiliko makubwa.

Takwimu

[hariri |hariri chanzo]

Mnamotarehe31 Desemba2023, Wakapuchini duniani walikuwa 9,684, kati yao mapadri 6.819. Mwaka 2011 walikuwa katika nchi 106:Afrika 1321;Amerika ya Kilatini 1720;Amerika ya Kaskazini 662;Asia-Oceania 2283;Ulaya 4378.[1]

Tanbihi

[hariri |hariri chanzo]
  1. Analecta Ordinis Fratrum Minorum Capuccinorum,Roma

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuWakapuchini kama historia yake au maelezo zaidi?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Wakapuchini&oldid=1442213"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2026 Movatter.jp