Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Wafinisia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Miji muhimu na njia za biashara za Wafinisia

Wafinisia (auWafoinike) walikuwa wakazi waFinisia ambao zamani zaNyakati za Kale waliishi kwenye mwambao wa mashariki waBahari ya Mediteranea.

Miji-dola yao ilikaa katika eneo la nchi za kisasa zaLebanoni naSyria.

Wafinisia walizungumzaKifinisia kilichokuwalugha ya Kisemiti ambayo ilipotea baada ya kusambaa kwaKiarabu tangukarne ya 7.

Walikuwa wafanyabiashara na mabaharia hodari sana. Walijenga utajiri wao juu yabiashara ya ubao kutoka milima ya Lebanoni. Hasa miti ya aina yaseda (Cedrus Libani) ilitafutwa sana.

Baadaye waliunda makoloni yao katika magharibi ya Mediteranea hadiHispania. Lakini koloni lao mashuhuri lilikuwaKarthago (Afrika ya Kaskazini).

Mafanikio ya kihistoria ya Wafinisia

[hariri |hariri chanzo]

Wafinisia (kama siWakananayo) walianzishamwandiko wa pekee uliokuwa chanzo chaalfabeti zote zaUlaya kupitiaalfabeti ya Kigiriki.

Mabaharia Wafinisia walikuwa watu wa kwanza waliozunguka bara laAfrika kwa jahazi zao. Safari hiyo ilitokea kama mwaka600 KK kwa niaba ya mfalmeNeko II wa Misri aliyewaajiri kwa safari ile.

Viungo vya Nje

[hariri |hariri chanzo]
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Wafinisia&oldid=1211304"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp