Milki za Mexiko wakati wa kufika kwa Wahispania 1519
Azteki ilikuwa jina la ustaarabu muhimu nchiniMexiko kabla ya kufika kwa Wahispania. Waazteki walitawala nyanda ja juu za Mexiko ya Kati pamoja na mji mkuuTenochtitlan uliokuwaJiji la Meksiko jinsi uanvyoitwa leo.
Waazteki ambai kiasili walikuwa wavindaji na wahamiaji walifika mnamo mwaka1325 kwenyeziwa la Texcoco kutoka kaskazini wakajenga makazi yao kwenye kisiwa ziwani wakaita mji "Tenochtitlan".
Askari Azteki; kengee za mikuki inakata kwa vipande vikali vya mawe magumu
Wafalme wa Azteki walipanusha eneo lao na hadi kufika kwa Wahispania mji mkuu ulikuwa na wakazi 300,000 ukiwa mji mkuu wa milki iliyotawala maeneo mapana katika nyanda za juu. Kitovu cha milki hii kilikuwa maungano ya miji mitatu ya Tenochtitlan, Texcoco na Tlacopan.
Mji mkubwa wa Tenochtitlan ulilishwa kwa kodi za maeneo yaliyotawaliwa na Waazteki. Mtindo wa utawala huo ulikuwa kudai malipo ya kodi baada ya kuwashinda majirani. Menginevyo mila, desturi na sheria ziliendelea kufuatana na utamaduni wa kila mahali.
Mtindo huu ulirahisihsa utawala kwa sababu uliwaachia watawaliwa kiwango kikubwa cha uhuru wa ndani lakini baadaye ilikuwa rahisi kwa Wahispania kupasua milki hii kwa kujiunga na vikundi vilivyotawaliwa.
Kilimo cha Waazteki kilitumia mazao kama vile mahindi, maharagwe, mboga na nyanya. Hawakufuga wanyama isipokuwa mbwa na kuku lakini maziwa ya nyanda za juu yaliwapa samaki. Mazao mengi yaliyo kawaida leo hii duniani yaligunduliwa na kustaawishwa na wakulima wa Amerika kabla ya kufika kwa Wahispania.
Teknolojia ya Azteki haikugundua bado matumizi ya chuma au shaba. Vifaa vyote vilikuwa vya ubao na mawe. Kwa visu na silaha walitumia mawe magumu sana ya obsidiani yaliyovunjwa na kuwa na kona kali. Silaha hizi hazikuweza kushindana na panga na kinga za chuma za Wahispania waliokuwa pia na aina za bunduki.
Mwaka1519 alifika MhispaniaHernan Cortes pamoja na jeshi ya askari 450 kutokavisiwa vya Karibi vilivyovamiwa na Hispania tangu siku zaKristoforo Kolumbus. Baada ya kupokelewa vizuri na mfalme wa AztekiMoctezuma II walimkamata mfalme kama mfungwa na kuchukua dhahabu kutoka mahekalu. Wenyeji wa mji waliwashambulia na kuua Wahispania wengi. Cortes aliweza kukimbia akarudi na jeshi mpya akaweza kuteka mji tar.13 Agosti1521 na kuuharibu kabisa.
Kuja kwa Wazungu kulisababisha vifo vingi hasa kutokana na magonjwa yasiyojulikana bado Amerika bara lakini pia kutokana na vita na utumwa.
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuAzteki kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.