Chuo ni taasisi yaelimu ya pekee. Inatoa mafunzo yakazi fulani. Mifano ni chuo chaufundi, chuo chakilimo au chuo chaualimu. Kwa kila namna chuo kinaanza kufundisha watu baada ya kumaliza ngazi fulani yashule.
Kiasili maana yaneno "chuo" ilikuwa sawa na "kitabu". Kwa maana hiyo linatumiwa kwa mfano katikatafsiri zaBiblia kama vileInjiliya Luka 4:17 "Yesu akapewa chuo cha nabii Isaya, akakifungua chuo".[1]
Kutokana na maana hii asilia "chuo" kimekuwa pia neno la kutaja mahali pa kujifunza kusoma, kwa hiyo katikaKiswahili cha miaka iliyopita kiliweza kutaja piashule.[2].
Leo hii matumizi ya neno yamebadilika, kwa maana ya "kitabu" hupatikana tu katika matini zenye Kiswahili cha zamani na kama mahali au taasisi ya elimu kwa jumla, neno "shule, skuli"[3] limechukua nafasi pana zaidi.
Jina la "Chuo" linaweza kutaja taasisi zinazotoa elimu kwa ngazi tofauti sana. Hii itategemea na muundo wa elimu katika nchi mbalimbali.
Chuo cha ufundi stadi, kwa mfanouseremala, mara nyingi kitafundishawanafunzi waliotokashule ya msingi na kuwafundisha ufundi fulani kama useremala, yaani matumizi ya vifaa vya fani hii na kuwawezesha kutengenezafenicha au kushughulikia kazi zinazohusu matumizi yaubao katikaujenzi.[4]
Vyuo vingine vinaweza kuwapeleka wanafunzi wao hadi ngazi yadiploma au hatabachelor.
Katika nchi kadhaa chuo kinatoaelimu ya juu lakini katika fani moja tu, tofauti nachuo kikuu kinachofundisha fani mbalimbali na pia kuweka uzito kwenye uchunguzi wa kitaalamu, si mafundisho pekee.
Watu wanaoingia katika chuo kwa shabaha ya kujifunza huitwa wanafunzi, pia wanachuo au wanazuo(ni). Wale wanaotoa elimu huitwawalimu, kwenye ngazi za juu zaidi wanaweza kuitwa piaprofesa au wakufunzi.
Nchini Tanzania vyuo huratibiwa na tume ya vyuo vikuu nchini humo inayoitwa TCU (Tanzania commission for university).[5] Tume ya vyuo vikuu Tanzania imeonyesha orodha ya vyuo nchini Tanzania kwamba mpaka mnamo waka 2019 Tanzania ilikua tayari na vyuo zaidi ya hamsini (50), Orodha ya vyuo vilivo idhinishwa ta tume ya vyuo vikuu nchini Tanzania(bofya hapa)Ilihifadhiwa 5 Desemba 2020 kwenyeWayback Machine..
↑Hii ni toleo la "Union version" (1952) linalofuata hapa tafsiri yaEdward Steere ya 1883; tafsiri za kisasa hutumia hapa "kitabu" badala ya "chuo". Tafsiri ya "Qurani TukufuIlihifadhiwa 13 Novemba 2017 kwenyeWayback Machine." ya Sheikh Ali Muhsin Al Barwani inatumia kote neno "kitabu", si "chuo".
↑A. C. Madan Swahili-English Dictionary Oxford 1903: "Chuo, n. {vy-), (i) book; (2) school" (online hapa)