Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Vita

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Vita: MfalmeRamses II mnamo 1274 KK, MfalmeGustav Adolf mnamo 1623, Faru ya Marekani M1 2005

Vita ni mapambano baina ya nchi,mataifa au angalau vikundi vikubwa vyawatu yanayoendeshwa kwa nguvu yasilaha.

Mchoro waPier Gerlofs Donia naWijerd Jelckama wakipigana kwa ajili ya uhuru wa watu.

Katika vita kuna pande mbili au zaidi. Husababisha mateso, vifo na kuharibika kwamali ya watu pamoja namazingiraasilia.

Mwanamgambo wa Kipalestina akiwa ameshika silaha aina yaM16 rifle, mwaka 2009.

Asili ya vita ilikuwa mapambano kwa silaha kati ya makabila au vijiji mbalimbali. Baada ya kutokea kwamadola ilikuwa zaidi serikali au watawala wa madola walioamua juu ya vita.

Mlipuko wa silaha ya nyuklia mwaka 1951.

Aina za vita

Kuna aina tofauti za vita:

  • vita kati yanchi mbili au zaidi kwa niaba yaserikali zao
  • vita vya wenyewe kwa wenyewe ndani ya nchi nzima kwa msingi wa itikadi au maslahi tofauti
  • vita ya uhuru ambako watu wa eneo fulani wanapambania dola ya pekee, kwa mfano
    • vita ya wenyeji wa koloni au nchi lindwa dhidi ya serikali ya kikoloni au nchi inayotawala
    • vita ya watu wa sehemu moja ya nchi dhidi ya serikali ya nchi nzima

Watekelezaji wa vita

Watekelezaji wa vita huitwaaskari auwanajeshi.Historia imejua vipindi ambapowanaume wote wa nchi fulani walitakiwa kushika silaha na kushiriki katika mapigano. Palikuwa pia na vipindi nautamaduni ambapo wapiganaji walikuwa watu wa pekee wenyejukumu hilo ama kwa sababu walipaswa kuwa askari kufuatana nasheria za nchi au kwa sababu walikodiwa kwakazi hii.

Wanajeshi rasmi huwa chini yakanuni za vita lakini sehemu kubwa na vita inashirikisha watu wasiofuata kanuni hizo kamawanamgambo hasa katika vita za wenyewe kwa wenyewe.

Silaha

Wanadamu wametumiaakili nyingi kuboresha vifaa vya vita, yaanisilaha, na mbinu za vita.Maendeleo ya silaha yamesababisha kupungua kwaidadi ya askari wanaopigana moja kwa moja lakini uharibifu wa silaha umeongezeka.

Silaha za kale zilitegemeanguvu yamkono wa mtu zikifikiaumbali mdogo. Silaha zimebadilika kulenga mahali ambapo ni mbali zaidi na zaidi. Silaha kali za kisasa zina uwezo wa kuharibu nchi yote; jumla yasilaha za nyuklia inatosha kuuauhai woteduniani.

Jitihada za kuepa au kupunguza athari za vita

Kutokana na uharibifu mkubwa unaosababishwa na vita palikuwa tena na tena na makubaliano juu ya kanuni za vita. Kanuni hizo hulenga kupunguza hasara inayosababishwa na mapigano. Lakini historia imejaa pia mifano ambapo kanuni hizo zilivunjwa au kupuuzwa.

Katikakarne ya 20 mataifa mengi yalipatana mikataba ya kimataifa juu ya kanuni za vita. Chanzo kilikuwaMapatano ya Geneva baada ya kuundwa kwaKamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu mwaka1863.

Baada yavita kuu ya kwanza ya dunia nchi nyingi ziliundaShirikisho la Mataifa kwa shabaha ya kuzuia vita lakini hii ilishindikana baada ya nchi kubwa kamaUrusi,Ujerumani naItalia kupuuza maazimio yake. Kuundwa kwaUmoja wa Mataifa kulikuwa jaribio jipya la kuwa nataasisi ya kimataifa yenye uwezo wa kuzuia vita.

Vasili Vereshchagin: Ufaulu wa Vita (1871)

Misemo juu ya vita

  • "Inawezekana kuanza vita unapotaka lakini haiwezekani kuimaliza unapotaka." -Niccolò Machiavelli
  • "Vita ni baba wa vitu vyote." -Heraklitos
  • "Vita ni aina ya siasa kwa kutumia mbinu tofauti." -Carl von Clausewitz
  • "Ukitaka amani andaa vita." -Vegetius
  • "Si vita, bali amani ni baba wa vitu vyote." -Willy Brandt
  • "Vita abadan!" -Yohane Paulo II
  • "Vita ilipokwisha askari alirudi nyumbani. Lakini alipokosa chakula akamwona mwenye chakula. Akamwua. "Lakini huruhusiwi kumwua mtu!" alisema hakimu. "Kwa nini?" aliuliza askari." -Wolfgang Borchert
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Vita&oldid=1398204"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp