Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Visiwa vya Marshall

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Aolepān Aorōkin M̧ajeļ
Republic of the Marshall Islands
Jamhuri ya Visiwa vya Marshall
Bendera ya Marshall IslandsNembo ya Marshall Islands
BenderaNembo
Kaulimbiu ya taifa: "Jepilpilin ke ejukaan"
Wimbo wa taifa:Forever Marshall Islands
Lokeshen ya Marshall Islands
Mji mkuuMajuro
7°7 N 171°4 E
Mji mkubwa nchiniMajuro
Lugha rasmiMarshallese,Kiingereza
Serikali
Hilda Heine
Uhuru
kutokaMarekani

21 Oktoba1986
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
181 km² (ya 213)
‘‘(kidogo sana)’’
Idadi ya watu
 -Julai 2009 kadirio
 -2021 sensa
 - Msongamano wa watu
 
68,000 (ya 205)
42,418
233/km² (ya 28)
FedhaUS Dollar (USD)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC+12)
(UTC)
Intaneti TLD.mh
Kodi ya simu+692

-


Visiwa vya Marshall ninchi ya visiwani yaMikronesia katikaPasifiki yamagharibi.

Nchi jirani katikabahari niNauru,Kiribati,Shirikisho la Mikronesia na eneo laMarekani laKisiwa cha Wake.

Atolli ya Majuro inashika nafasi yamji mkuu.

Jiografia

[hariri |hariri chanzo]

Eneo la visiwa vya Marshall nisafu mbili za visiwa au atolli zinazoelea sambamba:

Kwa jumla kuna visiwa na vipande vya atolli 1,150 katika eneo la bahari lakm² 1,900,000.

Historia

[hariri |hariri chanzo]

Jina limetokana nanahodhaMwingerezaJohn Marshall aliyetembelea eneo hili mwaka1788 na kulichora katikaramani. Ingawa visiwa vilikaliwa tayari tangukarne nyingi na watu kutokaMikronesia lakinijina la Kizungu limebaki kwa ajili ya jumla ya visiwa.

Mwisho wakarne ya 19Ujerumani ulianzishaukoloni juu ya visiwa ukaviunganisha kiutawala naGuinea Mpya ya Kijerumani.

Katikavita kuu ya kwanza ya dunia vilitwaliwa naJapani iliyoendelea kutawala visiwa kamaeneo lindwa kwa niaba yaShirikisho la Mataifa.

Baada yavita kuu ya pili ya dunia vilikuwa chini yaMarekani.

Mwaka1979 visiwa vimepatamadaraka ya kujitawala na hatimaye kupokeauhuru kufuatana naazimio laUmoja wa Mataifa mwaka1990.

Majaribio ya kinyuklia

[hariri |hariri chanzo]

Kuanzia mwaka1946 Marekani ilitumia visiwa kwa ajili ya majaribio yamabomu ya nyuklia.

Hadi mwaka1958 ilitokea milipuko 6,913 kwenye atolli zaBikini naEniwetok. Hadi leo kuna wakazi wa visiwa wanavyoteswa namaradhi yaliyosababishwa namnururisho wa mabomu haya. Bikini haitawezekana kukaliwa na watu kabla ya mwaka2050, Eniwetok haifai kwa makazi yabinadamu kwa miaka 24,000 inayokuja.

Watu

[hariri |hariri chanzo]

Wakazi ni 68,000, wengi wakiwa wametokana na wenyeji wa kwanza.

Upande wadini, wengi niWakristo, hasaWakalvini (51.5%),Wapentekoste,Wakatoliki, mbali yaWamormoni (8.3%).

Tazama pia

[hariri |hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons


Nchi_na maeneo yaAustralia na Pasifiki
Australia |Fiji |Guam |Hawaii |Kaledonia Mpya |Kiribati |Kisiwa cha Pasaka |Mikronesia |Nauru |Nyuzilandi |Niue |Pitcairn |Polinesia ya Kifaransa |Palau |Papua Guinea Mpya |Samoa |Samoa ya Marekani |Visiwa vya Cook |Visiwa vya Mariana ya Kaskazini |Visiwa vya Marshall |Visiwa vya Solomon |Tonga |Tuvalu |Vanuatu |Wallis na Futuna
Makala hii kuhusu eneo fulani bado nimbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.

Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Visiwa_vya_Marshall&oldid=1315579"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp