Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Visiwa vya Aland

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Aland

Visiwa vya Aland(kwaKiswidi: Åland; kwaKifini: Ahvenanmaa) nifunguvisiwa laBahari ya Baltiki upande wakusinimagharibi waUfini.

Mji mkuu niMariehamn kwenyekisiwa chaFasta Åland.

Ndani ya Ufini ni jimbo lenyeutamaduni wa Kiswidi lililo na hali ya pekee kikatiba na kiwango kikubwa cha kujitawala.

Funguvisiwa lina visiwa zaidi ya 6,000: vingi ni vidogo sana na 60 pekee vinawatu. Jumla ya wakazi ni 26,530.

Umbali na Ufini nikilomita 15 na Uswidi ni km 40.

Kisiwa kikubwa ni Fasta Åland upande wa magharibi. Eeno la visiwa vyote nikm² 1,554.

Historia

[hariri |hariri chanzo]

Tangumwaka1000BK visiwa vilikuwa chini yaUswidi. Wakati wa Uswidi kutawala Ufini vilihesabiwa pamoja na jimbo la Kifini la Uswidi.

Tangu mwaka1809 vilihamishwa chini yaUrusi pamoja na Ufini wote.

Baada yavita kuu ya kwanza ya dunia kulitokeauhuru wa Ufini pamoja na fitina kama visiwa vitakuwa sehemu ya Ufini au ya Uswidi.

Shirikisho la Mataifa liliamua mwaka1920 ya kuwa

  • visiwa vitabaki sehemu ya Ufini
  • wakazi wawe na uhuru wa kutumialugha yao ya Kiswidi na kutunza utamaduni wao
  • visiwa viwe eneo bilawanajeshi

Ufini ilitekeleza azimio hili kwasheria mbalimbali. Hivyo Aland ni sehemu ya Ufini ambakolugha rasmi pekee si Kifini bali Kiswidi. Wafini kutokabara hawaruhusiwi kununuaardhi aunyumba moja kwa moja kama hawajaishi visiwani kwa miaka kadhaa kwanza.

Nchi huru
Nchi zisizokubaliwa
na umma wa kimataifa
Maeneo yanayojitawala
chini ya nchi nyingine
1 nchi yaAsia ya Magharibi kijiografia ambayo huhesabiwa kuwa sehemu yaUlaya kiutamaduni2nchi ya kimabara
Makala hii kuhusu maeneo yaUlaya bado nimbegu.
Je unajua kitu kuhusuVisiwa vya Aland kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Makala hii kuhusu maeneo yaUfini bado nimbegu.
Je unajua kitu kuhusuVisiwa vya Aland kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Visiwa_vya_Aland&oldid=1310016"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2026 Movatter.jp