Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Fidla

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutokaViolin)
Fidla ya kisasa.
Mpiga fidla waTanzania.

Fidla (kutokaKiingerezafiddle; pia:violini, kutokajina laKiitaliaviolino) niala ya muziki yenyenyuzi.Idadi ya nyuzi ni 4 zinazopigwa au zaidi kuchuliwa kwauta. Nyuzi zinawekwa kwa kawaida kwanoti za G, D, A na E.

Muundo wa fidla na matumizi yake

[hariri |hariri chanzo]

Fidla hufanywa kwamwili wamwangwi nashingo.Nyaya hufungwa juu kwenye shingo na hapo zinaweza kukazwa kwahesi. Upande wa juu wa mwili kunamashimo mawili yenyeumbo la S nyembamba.

Fidla inashikwa namchezaji baina yabega nakidevu.

Kwa kawaidamkono wa kuume hushika uta na kuiteleza kwenye waya na hivyo kutoasauti. Uta ni kamaupinde na kunariboni kati yancha za upinde. Riboni hufanywa kwanywele zafarasi.

Vidole vya mkono mwingine husogeza juu ya nyaya na kubadilisha sauti kwa kukaza waya mahali mbalimbali.

Kyoko Yonemoto anapiga Paganini.

Historia ya fidla

[hariri |hariri chanzo]

Fidla zilibuniwa katikaUlaya ya Kusini takriban miakaelfu iliyopita kama nakala ndogo za ala za nyaya kubwa zaidi.

Fidla kwa umbo la kisasa zimepatikana tangukarne ya 16 na mwanzoni zilikuwa na nyaya 3 pekee, lakini tangu mnamomwaka1600 zilikuwa karibu sawa na ala za leo.Maendeleo hayo yalitokea katikaItalia kaskazini. Baadaye mabadiliko madogo yaliendelea kufanywa.

Mafundi mashuhuri waliotengeneza fidla walikuwa pamoja nafamilia zaStradivari,Guarneri naAmati katika Italia za karne za 16 hadi18 hukoBrescia naCremona na akinaJakob Stainer hukoAustria. Ala zilizotengenezwa nao zinatafutwa hadi leo na kutumiwa kwa muziki wa kihistoria.

Watunzi muziki wote mashuhuri waUlaya walitunga muziki kwa ajili ya fidla, ama katikaokestra ama kama ala ya pekee.

Kadiri fidla ilivyopendwa, idadi ya wapiga fidla iliongezeka pamoja na mahitaji ya idadi kubwa ya ala. Kwa hiyo fidla zabei nafuu zilitengenezwa katikaviwanda vidogo. Mwaka1888 kiwanda cha kwanza cha fidla kilianzishwa nchini Japani.

Marejeo

[hariri |hariri chanzo]
  • Viol and Lute Makers of Venice 1490 -1630, by Stefano Pio (2012), Venezia Ed. Venice research,ISBN 978-88-907252-0-3
  • Violin and Lute Makers of Venice 1640 - 1760, by Stefano Pio (2004), Venezia Ed. Venice research,ISBN 978-88-907252-2-7
  • Liuteri & Sonadori, Venice 1750 - 1870, by Stefano Pio (2002), Venezia Ed. Venice research,ISBN 978-88-907252-1-0
  • The Violin Forms of Antonio Stradivari, by Stewart Pollens (1992), London: Peter Biddulph.ISBN 0-9520109-0-9
  • Principles of Violin Playing and Teaching, by Ivan Galamian (1999), Shar Products Co.ISBN 0-9621416-3-1
  • The Contemporary Violin: Extended Performance Techniques, by Patricia and Allen Strange (2001), University of California Press.ISBN 0-520-22409-4
  • The Violin: Its History and Making, by Karl Roy (2006), ISBNISBN 978-1-4243-0838-5
  • The Fiddle Book, by Marion Thede (1970), Oak Publications.ISBN 0-8256-0145-2
  • Latin Violin, by Sam Bardfeld,ISBN 0-9628467-7-5
  • The Canon of Violin Literature, by Jo Nardolillo (2012), Scarecrow Press.ISBN 0-8108-7793-7
  • The Violin Explained - Components Mechanism and Sound by James Beament (1992/1997), Clarendon Press.ISBN 0-19-816623-0
  • Antonio Stradivari, his life and work, 1644-1737', by William Henry Hill; Arthur F Hill; Alfred Ebsworth Hill (1902/1963), Dover Publications. 1963. OCLC 172278.ISBN 0-486-20425-1
  • An Encyclopedia of the Violin, by Alberto Bachmann (1965/1990), Da Capo Press.ISBN 0-306-80004-7
  • Violin - And Easy Guide, by Chris Coetzee (2003), New Holland Publishers.ISBN 1-84330-332-9
  • The Violin, by Yehudi Menuhin (1996), Flammarion.ISBN 2-08-013623-2
  • The Book of the Violin, edited by Dominic Gill (1984), Phaidon.ISBN 0-7148-2286-8
  • Violin-Making as it was, and is, byEdward Heron-Allen (1885/1994), Ward Lock Limited.ISBN 0-7063-1045-4
  • Violins & Violinists, by Franz Farga (1950), Rockliff Publishing Corporation Ltd.
  • Viols, Violins and Virginals, by Jennifer A. Charlton (1985), Ashmolean Museum.ISBN 0-907849-44-X
  • The Violin, by Theodore Rowland-Entwistle (1967/1974), Dover Publications.ISBN 0-340-05992-3
  • The Early Violin and Viola, by Robin Stowell (2001), Cambridge University Press.ISBN 0-521-62555-6
  • The Complete Luthier's Library. A Useful International Critical Bibliography for the Maker and the Connoisseur of Stringed and Plucked Instruments byRoberto Regazzi, Bologna: Florenus, 1990.ISBN 88-85250-01-7
  • The Violin, by George Dubourg (1854),Robert Cocks & Co.
  • Violin Technique and Performance Practice in the Late 18th and Early 19th Centuries, by Robin Stowell (1985), Cambridge University Press.ISBN 0-521-23279-1
  • History of the Violin, by William Sandys and Simon Andrew (2006), Dover Publications.ISBN 0-486-45269-7
  • The Violin: A Research and Information Guide, by Mark Katz (2006), Routledge.ISBN 0-8153-3637-3
  • Per gli occhi e 'l core. Strumenti musicali nell'arte by Flavio Dassenno, (2004) a complete survey of the brescian school defined by the last researches and documents.
  • Gasparo da Salò architetto del suono by Flavio Dassenno, (2009) a catalogue of an exhibition that give complete informations on the famous master life and work, Comune di Salò, Cremonabooks, 2009.
  • Grillet, Laurent (1901). "Les ancetres du violon v.1". Paris.{{cite journal}}:Cite journal requires|journal= (help);Invalid|ref=harv (help)

Kujisomea

[hariri |hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Fidla&oldid=1194240"
Jamii:
Jamii iliofichwa:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp