Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Viktoria wa Uingereza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Malkia Victoria
Malkia Victoria mnamo mwaka 1882
AmezaliwaAlexandrina Victoria
24 Mei 1819
Kasri ya Kensington, London,Ufalme wa Muungano
Amekufa22 Januari 1901 (miaka 81)
Kasri la Osborne, Kisiwa cha Wight,Ufalme wa Muungano
Sababu ya kifoKiharusi
ElimuElimu ya kifalme kupitia waalimu wa nyumbani
Kazi yakeMtawala wa kifalme
NdoaPrince Albert wa Saxe-Coburg and Gotha (waliofunga ndoa: 1840–1861)
WatotoWatoto 9, wakiwemoMfalme Edward VII, Viktoria, Binti wa Kifalme Mkuu, naPrincess Alice
WazaziPrince Edward, Duke wa Kent na Strathearn
Princess Victoria wa Saxe-Coburg-Saalfeld

Malkia Viktoria (24 Mei181922 Januari1901) alikuwamalkia waUfalme wa Muungano waBritania naEire ya Kaskazini tangu1837 hadi1901. Hakukuwa namfalme au malkia mwingine aliyeshika nafasi ya mkuu wadola kwa muda mrefu zaidi hadi alipopitwa naElizabeti II.

Alipewahadhi ya malkia akiwa naumri wa miaka 18.William IV aliyekuwa mfalme alipofariki Viktoria amekuwamrithi kwa sababubaba yake alikuwa ameshaagadunia.

Alipokuwa malkiaUingereza ilikuwa tayariufalme wa kikatiba namadaraka ya mfalme au malkia yameshapungua. Lakini aliheshimiwa sana akawaishara yamaendeleo na enzi ya Uingereza. Wakati wake nchi iliendelea kuwa yenye nguvu duniani na kujengautawala juu yamakoloni mengi.Mapinduzi ya viwanda yalifikiakilele chake na Uingereza ilishinda nchi zote za duniakiteknolojia,kiuchumi nakijeshi.

Kwenye mwisho wa utawala wake uwezo huu umeshapungua kutokana na maendeleo ya nchi kamaUjerumani naMarekani lakini alisimamiamilki iliyounganishatheluthi moja yawatu wote duniani sehemu yatano (20%) ya uso wa dunia.

Kipindi chake huitwa mara nyingi "enzi ya Viktoria".

Mwaka1840 aliolewa naAlbert wa Saksonia-Coburg na Gotha akazaliana nayewatoto 9. Albert aliaga dunia mapema mwaka1861 akiwa na miaka 42 pekee na Viktoria aliendelea kuonyeshahuzuni yake kwa kuvaanguo zamjane kwa miaka mingi iliyofuata.

Wakati Uingereza ilipopanua utawala wake duniani alipewa piacheo chakaisari chaUhindi.Binti yake wa kwanza aliolewa na KaisariWilhelm II wa Ujerumani.

Kipindi chake kilikuwa kipindi cha maendeleo ya kiuchumi na matabaka ya juu na ya kati yaliona maendeleo makubwa maishani lakini matabaka ya chini bado yalikuwa namaisha magumu. Hata kama jeshi la Uingereza ilipiganavita vingi duniani katika makoloni yake watu wa Uingereza yenyewe waliona kipindi kirefu chaamani na maendeleo.

Makala hii kuhusu mtu huyo bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuViktoria wa Uingereza kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Viktoria_wa_Uingereza&oldid=1425681"
Jamii:
Jamii zilizofichwa:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp