Mifano |
---|
- Mary anaimbavizuri
- Wafanyabiashara wanauzajumla
- Ndondi si mchezo mzurisana
- Kidawa anatembeaharakaharaka
- Joshua anakulapolepole
|
Kielezi (alama yake yakiisimu ni:E, ing.adverb) nineno aumaneno yanayotoa taarifa ihusuyokitenzi. Maneno hayo (vielezi)huelezea/hufafanua nakupambanua au kuongeza maana zaidi ya namna au jinsi tendo linavyotendeka - idadi au kiasi cha kutendeka kwa tendo hilo, mahali ambapo tendo linatendeka.
Hivyo basi kielezi ni neno au maneno yanayotoa taarifa ili kukujulisha kuwa kitenzi hicho kimetendekanamna gani au jinsi gani,mara ngapi au kwa kiasi gani,wapi,lini na kwa sababu gani.
Wakati mwingine vielezi hutoa taarifa inayohusu nomino, viwakilishi, vivumishi na hata vielezi vyenzake.
Uchambuzi
Mifano ya jumla
- Mtotohuyu analiasana (mtoto =nomino, huyu =kivumishi, analia =kitenzi kikuu, sana =kielezi cha namna au jinsi ambavyo huyo mtoto kilizi analia).
- Kassimanatembeakitoto (Kassim =nomino, anatembea =kitenzi kikuu, kitoto =kielezi cha namna au jinsi huyo Kassim anavyotembea kitoto).
- Chakulakimepikwamara mbili (chakula =nomino, kimepikwa =kitenzi kikuu, mara mbili =kielezi cha idadi au kiasi, yaani mara mbili).
- Wanafunziwamodarasani (wanafunzi =nomino, wamo =kitenzi kishirikishi, darasani =kielezi cha mahali)
- Mvuaimenyeshaleomchana (mvua =nomino, imenyesha =kitenzi kikuu, leo =kielezi cha wakati, mchana =kielezi cha wakati
- Stevealikwendadukani usiku (Steve =nomino, alikwenda =kitenzi kikuu, dukani =kielezi cha mahali, usiku =kielezi cha wakati)
- Mariamu alizaliwawakati wa ukoloni (Mariamu = nomino, alizaliwa =kitenzi kikuu, wakati wa ukoloni =kitenzi cha wakati
Aina za vielezi
- Vielezi vya namna au jinsi
- Vielezi vya idadi au kiasi
- Vielezi vya mahali au sehemu
- Vielezi vya wakati au muda
Vielezi vya namna au jinsi
Huelezea jinsi au namna jambo linavyotendeka.
Vielezi vya idadi au kiasi
Huelezea kitendo kilifanyika mara ngapi.
Vielezi vya mahali au sehemu
Huelezea kitendo kilifanyika sehemu gani.
Vielezi vya wakati au muda
Huelezea zaidi wakati au muda kitendo kinapofanyika, kwa mfano:jioni,usiku,asubuhi n.k.
Tazama pia
 | Makala hii kuhusu mambo yalugha bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuVielezi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari. |