Alpaka ni mnyama wa kufugwa waspishiVicugna pacos katikafamilia Camelidae, anayeishiAmerika Kusini. Alpaka anafanana nalama mdogo, lakini ameainishwa katika jenasi tofauti. Kuna nususpishi mbili za alpaka; alpaka suri na alpaka huacaya.
Kwa kawaida, alpaka mzima ana kimo cha sm 81–99 mabegani, na uzito wa kilo 48–84.
Alpaka hutunzwa kwa makundi na hulishwa katika nyanda za juu za milima yaAndes katika upande wa kusini waPeru, kaskazini yaBolivia,Ekuador, na kaskazini yaChile, ambako wanaishi mita 3,500–5,000 juu ya usawa wa bahari, mwaka wote.[1] Alpaka ni wadogo kiasi kuliko lama, na tofauti na lama, hawakufugwa kuwa wanyama wa mizigo, badala yake walifugwa mahususi kwa ajili ya manyoya yao. Manyoya ya alpaka hutumiwa kutengeneza vitu vifumwavyo, mithili ya sufu. Vitu hivyo ni pamoja na mablanketi, sweta, kofia, glavu na nguo nyingine katika Amerika Kusini, na sweta, soksi, koti na matandiko katika sehemu nyingine duniani. Fumwele za manyoya yao zinapatikana katika zaidi ya rangi 52, kama zinavyoainishwa Peru.
Katika biashara ya vitambaa, maana ya msingi ya "alpaca" ni nywele za alpaka wa Peru lakini, kwa upana zaidi, "alpaca" inamaanisha mtindo wa vitambaa vilivyotengenezwa awali kutoka nywele za alpaka, ambavyo sasa vinatengenezwa mara nyingi kwa fumwele zinazofanana na nywele za alpaka, kama sufu za ubora sana.