VP Records | |
---|---|
![]() | |
Imeanzishwa | 1979 |
Mwanzilishi | Vincent "Randy" Chin Patricia Chin |
Nchi | United States |
Mahala | Queens, New York |
Tovuti | Official website |
VP Records ni jina la studio ya kurekodi muziki waReggae inayojisimamia ambayo inapatikana mjiniQueens, New York. Inajulikana sana kwa kuwatayarishia muziki waimbaji wengi waKikaribi.
VP Records ni lebo iliyoanzishwa mnamo 1979 na marehemuVincent "Randy" Chin na mkewe Patricia Chin,Wajamaica wenye asili yaKichina ambao walikuwa wakimiliki lebo yaRandy's Records MjiniKingston, Jamaica (inavyoonekana katika filamu ya ‘’Rockers’’) na piaStudio 17. Katika ti ya miaka ya 1970s wawili hawa walihamia Jiji laNew york, huku wakianzisha duka la kuuza rekodi mjiniBrooklyn liitwaloVP Records mnamo 1975, mahali ambapo waliuza na kusambaza rekodi kutoka huko. Mnamo 1979 walihamisha makao ya gala hilo la muziki kwendaQueens, Jamaica. Mnamo 1993, lebo ya rekodi ilianzishwa baada ya duka la rekodi kunawili. Jina la lebo limetokana na nukta za kwanza za majina ya waanzilishi.
Lebo hii ilijiimarisha kuwa moja kati ya lebo huru kubwa zaidi kwa muzikiwa mienendo ya Reggae na dancehall. Kwa umaarufu wa sauti yariddim kutoka mapema mwaka wa 2000, lebo hii ilileta ufanisi mkuu kwa wasanii wengi katika dunia nzima kama vileSean Paul kupitia kwa mikataba ya lebo na lebo yaVirgin MusicCanada naAtlantic Records inayomilikiwa na Warner Music. Lebo hii maranyingi huhusishwa na umaarufu mkubwa waElephant Man ambaye pia anajilikana kama ‘’Energy God’’ au ‘’Ele’’ kupitia kazi yake naBad Boy Records. Nembo ya VP Records ni “Maili mbele katika muziki wa Reggae”. Kando na reggae, VP pia inajulikana kwa mwenendo wadancehall naSoca. VP pia ilitoa mshururu wa albamu ambazo zinajikitha katika sauti za ‘’Riddims’’, ambazo zinashirikisha wasanii mbalimbali.
VP imewahi kushindatuzo la Billboard kama lebo huru bora zaidi (Best Independent Label) kwa miaka miwili ma pia imepokea tuzo la Lebo bora zaidi ya Reggae kwa miaka mitatu mtawalia. Pia ilifuzu kwa tuzo la ‘’Best Independent Reggae Label’’ la 2003 la Billboard Hip-Hop and R&B, na pia ilikuwa imetajwa na kushirikishwa katika machapisho kamaVibe magazine,New York Times,Los Angeles Times,Billboard, naTime magazine.
Lebo hiyo sasa inasimamiwa na wana wa Bw.Chin, Randy na Christopher huku Bi Patrici Chin akiendelea kutoa usaidizi wa kuendelea kuitunza kampuni hii ya marehemu mumewe.
Wengi wa wasanii wa lebo hii wamehusika katika utata kutokana na maneno ya nyimbo zao ambayo huchochea vurugu (ukiwemo uuaji) dhidi wale wanaojihusisha kimapenzi kati ya jinsia moja.