Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

V-2

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Roketi ya V-2 iliyohiadhiwa kwenye eneo la makumbusho ya Peenemünde, Ujerumani

V-2 (kifupi chaKijerumaniVergeltungswaffe 2, yaani "silaha ya kulipiza kisasi namba mbili") ilikuwaroketi yakijeshi yaUjerumani wakati waVita Kuu ya Pili ya Dunia. Ilikuwa chombo cha kwanza kilichotengenezwa nabinadamu kilichofikiaanga-nje.

Roketi zote za kisasa hufuata kimsingi mfano wa V-2. Ilibuniwa nawahandisi wa kijeshi nawanasayansi chini yauongozi waWerner von Braun kwenye kituo cha kijeshi chaPeenemünde kwenyemwambao waBahari Baltiki. Ikarushwa mara ya kwanzatarehe3 Oktoba1942 ikifikiakimo chakilomita 84.5. Tarehe20 Juni1944 ilifikia kimo cha kilomita 174.6 na kuvuka mpaka wa anga-nje uliopo kwa kilomita 100.

Kusudi la kubuni V-2 lilikuwa kubebamabomu kwamiji yaUlaya, hasaUingereza, ambakojeshi la anga la Ujerumani lilikutana na upinzani mkali wa Waingereza. V-2 za kwanza zilizotumiwa kama silaha zilipigaParis naLondon tarehe8 Septemba 1944. Zaidi ya V-2 3000 zilirushwa na jeshi la Kijerumani dhidi ya shabaha za wapinzani wake zikaua takribanwatu 7,200.

Baada yavitaWamarekani naWarusi walikamatawataalamu wa Peenemünde na kuwatumia kuanzisha miradi ya roketi kwao. Kwa njia hii Werner von Braun aliendelea kuwamkurugenzi wa kituo chaMarshall Space Flight Center akaitwa "Baba wa miradi ya anga-nje".

Makala hii kuhusu mambo yateknolojia bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=V-2&oldid=1308724"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp