Historia ya V ina asili za pamoja na U, W, Y na F. Historia hii ni ngumu kidogo kwa sababu alama ilipita katika alfabeti za lugha ambazo zilitumia hasa alama hii kwa sauti tofautitofauti. Kwa sababu hii matamshi yalibadilika kati ya lugha na lugha. Pia lugha mpya iliweza kuona haja ya kuunda alama mpya kwa sauti ya pekee.
Alama ya V kiasili ilimaanisha sauti za "v" na "u" kwa pamoja katika Kilatini cha Kale. Iliandikwa kama V na matamshi yake yalitegemea nafasi yake katika neno pia lahaja mbalimbali. Tofauti ilikubwaliwa tu wakati wa Kilatini Kipya katika karne ya 16 ambako wataalamu wa Ulaya walikubaliana kutumia alama yenye kona V kwa sauti yakonsonanti na alama isiyo na kona U kwavokali.
Wafinisia walikuwa na "waw" iliyokuwa kiasili picha iliyorahisishwa ya fimbo la kingoe au kiopoo. Wagiriki wa Kale walichukua alama hiyo na kuitumia kwa namna mbili: kwa umbo moja kamadigamma (tazamaF) na umbo la pili kama "ipsilon" bila kujali maana asilia ilitaja sauti kati ya "u" na "i".
Waitalia ya kwanza wakaendelea kutumia alama kwa aina ya "u" lakini pia "v" kama ilikuwa mwanzoni wa neno. Waroma walipokea vile.