Uaji katika nyumba - taswira ya Jacub Schikaneder (1890)
Uuaji (kwaKiingereza:homicide) kwa macho yasheria ni tendo la mtu mmoja linalosababishakifo cha mtu mwingine.
Uuaji kwa maana hiyo unahitaji tendo la mtu ambalo limelengwa, unaweza kutokana kwa bahati mbaya, kwa kutojali au kupuuza hata bila nia ya kusababisha hasara, au kwa kusudi.
Kisheria mauaji huangaliwa kwa namna tofauti zinazoweza kutofautiana kati ya nchi na nchi kufuatana na mifumo mbalimbali ya sheria, kama nijinai au la. Namna hizo ni pamoja nakuua bila kukusudia (Kuuwa bila kunuia, ing.manslaughter) aukuua kwa kukusudia (Kuua kwa kunuia, ing.murder)[1], kujitetea, kujilinda, kuuavitani, kuua kwaamri ya wakubwa, au kutekelezaadhabu ya kifo.
Sheria zinazofuata mapokeo ya Sheria ya Kiroma zinatofautisha mara nyingi kati ya mauaji yanayotekelezwa kwa kukusudia na bila kukusudia; sheria za nchi kamaMarekani hutofautisha kati ya ngazi au uzito tofauti wa uuaji kwa kukusudia (first - second degree murder) ambayo haipo katika sheria zinazofuata mapokeo yaUingereza kamaTanzania.
Kwa jumladini zinakataza uuaji kamadhambi kubwa, ingawa si kila mara, hasa katika juhudi za kujihami dhidi ya mvamizi.
↑Wakati wa kutunga makala hii kwenye Februari 2021 msamiati wa sheria ya jinai haujaamuliwa bado nchini Tanzania; kuna tafsiri tofauti ya istilahi za Kiingereza
Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuUuaji kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.