Sehemu kubwa ya mmeng'enyo wachakula inatokea hapa, yaani ni katika sehemu hii kwamba mwili unatoa virutubishi vyake kutokaujiuji wa chakula kilichotafunwamdomoni na kupasuliwakikemia tumboni.
Inapokeakiowevu chanyongo na chakongosho kwa njia ya kipito cha nyongo. Upande wa ndani wa utumbo huwa na mikunjo mingi pamoja na vili ambayo ni vimbe kamavidole vidogo vyote vinayoongeza eneo linalopatikana kwa mmeng'enyo wa chakula.
Ujiuji wa chakula unatoka kwenye tumbo na kuingia katika sehemu ya duodeno lenye urefu wasentimita 24. Hapa kiwango chaasidi katikatope la chakula kinapunguzwa.
Katika jejuno kiowevu cha kongosho kinapasuawanga,protini namafuta kwa sehemu zinazoweza kupokewa na damu. Kiowevu cha nyongo kinasaidia upasuaji wa mafuta.Molekuli zinazopatikana baada ya hatua hiyo zinapita katikangozi ya utumbo na kupelekwa katikaini ambako zinashughulikiwa tena. Utumbo mwembamba unapokea pia sehemu kubwa yamaji yanayohitajika mwilini na kuiondoa katika tope la chakula.
Katika sehemu ya ileo ni hasavitamini zinazopokewa na kupitishwa kwenda damu.
Kutoka hapo mabaki ya chakula yanaendelea katikautumbo mpana.
Makala hii kuhusu mambo yaanatomia bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuUtumbo mwembamba kama matumizi yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.