Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Utatu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha takatifu inayodokezafumbo la Utatu kwa kuchoramalaika watatu waliolakiwa naAbrahamu hukoMambre. Ilichorwa nammonakimtakatifuAndrej Rublëv (1360-1427) na kwa sasa inatunzwaMoscow,Tretjakow Gallery.
Mchoro waKilatini unaofafanua umoja wa Mungu na tofauti za nafsi zake tatu katika mafungamano yao.
Sehemu ya mfululizo kuhusu
Ukristo
Yesu Mchungaji mwema.

Utatu auUtatu mtakatifu ni hali ya kuwa Watatu katikaumoja kamili.

Jina hilo la kiteolojia linatumika hasa kufafanuliaimani yaWakristo wengi kwambaMungu pekee, sahili kabisa, niNafsi tatu zisizotenganika kamwe:Baba,Mwana naRoho Mtakatifu.

Katika Biblia

[hariri |hariri chanzo]

Kwa agizo laYesu watakaomuamini wanatakiwakubatizwa kwa jina la hao watatu (Injili ya Mathayo 28:19). Agizo hilo la mwisho lilifuata na kujumlisha mafundisho yake mbalimbali kuhusu Baba, kuhusu yeye mwenyewe kama Mwana na kuhusu Roho Mtakatifu.

Ufafanuzi wa teolojia

[hariri |hariri chanzo]

Umoja wa Nafsi hizo unatokana naasili yake pekee, yaani Baba ambaye ndani mwake anamzaamilele Mwana kamamwanga toka kwa mwanga, kamaNeno au Wazo lake (Hekima), tena anamvuvia Roho Mtakatifu kamaUpendo ambao unamuunganisha na Mwana na kukamilisha umoja wao[1].

Kimsingi ni kwamba Mungu pekee (Baba) anajifahamu milele (Mwana) na kwa kujifahamu anajipenda (Roho Mtakatifu).

Katika matamko rasmi ya Kanisa

[hariri |hariri chanzo]

Imani hiyo ilizidi kufafanuliwa hasa katikakarne IV,mitagusomikuu ya kwanza ilipochukua msimamo dhidi yawazushi waliokanushaumungu wa Yesu na wa Roho Mtakatifu. Ilipata muundo wa kudumu katikaKanuni ya Imani ya Nisea-Konstantinopoli inayotumika hadi leo katikamadhehebu mengi yaUkristo.

Kwa imani hiyo tunapaswa kusadiki hasa Utatu wa Mungu pekee, kwamba ni Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Milele yote Baba kwa jinsi alivyo ndani mwake anamzaa Mwana na kumvuvia Roho Mtakatifu, kama vile jua linavyotoa mwanga na joto lisitenganike navyo. Mwana, ambaye “ni mng’ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake” (Eb 1:3), alisema: “Nimekuja kutupa moto duniani” (Lk 12:49). Naye Roho aliwashukia wafuasi wake “kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu” (Mdo 2:3-4).

Mungu hagawanyiki hata kidogo, bali daima niUmoja kamili. “Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja” (Mk 12:29).Tumuabudu yeye peke yake katika nafsi tatu, na Utatu wa nafsi katika Umoja wa hali yake, tusichanganye nafsi wala kugawa Umungu. Baba si Mwana wala Roho Mtakatifu. Mwana si Baba wala Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu si Baba wala Mwana. Lakini milele yote nafsi hizo tatu ni Mungu yuleyule pasipo tofauti ya kuzitenganisha: kila moja imo ndani ya nyingine. “Mimi na Baba tu umoja” (Yoh 10:30).

Tumejua kuwa Mungu ni Umoja wa nafsi tatu kwa sababu Baba aliwatuma kwetu Mwanae na Roho Mtakatifu. “Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake. Na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, ‘Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye’” (Math 3:16-17). Naye akaagiza, “Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu” (Math 28:19). Ni nafsi tatu zenyejina moja, yaani Umungu mmoja tu.

Umoja wa Mungu unategemea hasa kwamba Mwana na Roho Mtakatifu wanachanga Umungu wa Baba, ambaye wanatokana naye pasipo utengano wowote. Baba anajifahamu na kujipenda: wazo analojifahamu ndiye Mwana, upendo anaojipenda katika wazo hilo ndiye Roho Mtakatifu. “Baba, hao ulionipa nataka wawe pamoja nami popote nilipo, wapate na kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa msingi ulimwengu” (Yoh 17:24).

Nafsi tatu za Mungu zina Umoja hata katika utendaji, kila nafsi akiuchangia kulingana na sifa yake maalumu ndani ya Utatu. Baba Mwenyezi sifa yake niUwezo. Mwana kama Neno la Baba sifa yake niHekima. Roho kamaPumzi yauhai ya Baba sifa yake niUpendo. Katika Uwezo wake Baba anafanya yote kwa Hekima na Upendo, hasa katikautume wa Mwana aliyefanyika mtu na katika utume wa Roho kama paji. “Amin, amin, nawaambia: Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda; kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo Mwana vilevile” (Yoh 5:19).

Katika liturujia

[hariri |hariri chanzo]

Fumbo hilo linaadhimishwa katikaliturujia yamadhehebu mbalimbali yaUkristo wa mashariki (siku yaPentekoste) na yaUkristo wa magharibi (Jumapili inayofuata).

Tazama pia

[hariri |hariri chanzo]

Tanbihi

[hariri |hariri chanzo]
  1. Pontifical Council for Promoting Christian Unity: The Greek and the Latin Traditions regarding the Procession of the Holy Spirit Archived 3 Septemba 2004 at the Wayback Machine. and same document on another site

Marejeo

[hariri |hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuUtatu kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Utatu&oldid=1332445"
Jamii:
Jamii iliofichwa:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp