Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Utando wa seli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Utando wa seli(extracellular: Nje ya seli;Lumen of cell: Ndani ya seli;hydrophilic: ya kukubali maji;hydrophobic: ya kukataza maji)

Utando wa seli ni rusu nyembamba kamangozi inayopakanaseli zaviumbehai.Majina yaKiingereza nicell membrane,plasma membrane aucytoplasmic membrane.

Kazi yake ni kutenganisha ndani na nje, yaani yaliyomo ndani ya seli na yale yalio nje yake.[1][2]

Kwa kila seli ni muhimu kukinga na kutenganishaplasma iliyopo ndani yake na athira aukemikali za nje. Seli zawanyama zinatenganishwa kati yao na utando wa seli pekee.

Kwenye seli zamimea,fungi nabakteria kuna piaukuta wa seli nje ya utando. Ukuta wa seli (ing.cell wall) unaimarisha seli, unaongeza kinga na kuwa kamafilta dhidi yamolekuli kubwa.

Utando wa seli unafanywa na safu mbili za molekuli zinazoitwa "fosfo-lipidi". Maana yake molekuli hizi zina sehemu yafosfati upande mmoja na sehemu yalipidi (mafuta) upande mwingine. Upande wa kifosfati inachanganya namaji lakini sehemu ya kimafuta inakataa maji. Kuna piaproteini nyingine zinazoweza kuongezwa ndani ya utando. Kwa njia hiyo seli inaweza kutawala nini iingie au kutoka.

Marejeo

[hariri |hariri chanzo]
  1. Kimball's biology pagesIlihifadhiwa 25 Januari 2009 kwenyeWayback Machine., Cell membranes
  2. Singleton P, (1999).Bacteria in biology, biotechnology and medicine (tol. la 5th). New York: Wiley.ISBN 0-471-98880-4.{{cite book}}: CS1 maint: extra punctuation (link)
Makala hii kuhusu mambo yabiolojia bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuUtando wa seli kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Utando_wa_seli&oldid=1467662"
Jamii:
Jamii iliofichwa:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp