Katikafani yahistoria "ustaarabu" (kwaKiingerezacivilization) ni hali yajamii iliyoendelea juu ya kuishi katikajumuiya ndogo zinazojitegema katika mahitaji yote. Kwenye hali ya ustaarabu watu wanashirikiana katika eneo kubwa zaidi, huwa na namna yaserikali.Shughuli zinagawanywa kati ya vikundi, matabaka nakazi mbalimbali chini yakanuni nasheria zinazosimamiwa na mtawala auserikali.
Miji ilitokea ambako sehemu ya watu haikuzalishavyakula bali kushughulika na kazi za pekee.
Mahitaji ya kusimamia na kupangakodi na mahitaji mengine yautawala yalisababisha kutokea kwambinu za kutunzakumbukumbu, hivyo vyanzo vya kuandika na kuhesabu.
Kwa maana hii "ustaarabu" hutazamiwa tofauti na maisha katika hali ya jumuiya ndogo ambako watu huishi katika koo ndogo za wakusanyaji, au makabila madogo yanayofuata zaidimila nadesturi lakini hawanamamlaka ya juu inayogharamiwa na wote.
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuUstaarabu kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.