Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Uskoti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uskoti
Scotland (Kiskoti)
Alba (Kigaeli)
Wimbo wa taifa: "Flower of Scotland" (hutumika zaidi)
Eneo la Uskoti katika Ufalme wa MuunganoEneo la Uskoti katikaUfalme wa Muungano
Mji mkuu
na mkubwa
Edinburgh
Lugha rasmi
  • Kiingereza
  • Kiskoti
  • Kigaeli cha Uskoti
  • Lugha ya Ishara ya Uingereza
Kabila
Dini
SerikaliBunge lenye mamlaka ya ndani chini ya muktadha wa kifalme wa kikatiba
  Mfalme
Charles III
  Waziri Mkuu wa Uskoti
John Swinney
Eneo
  Jumlakm2 80,231
Idadi ya watu
  Kadirio la 20225,439,842
  Msongamano70/km2
PLT (Kawaida)Kadirio la
  Jumla£218.0 bilioni
  Kwa kila mtu£39,707
HDI (2022)0.933juu sana
SarafuPauni ya Uingereza (GBP)
Majira ya saaUTCUTC+0 (GMT)
Upande wa magariKulia
Msimbo wa simu++44
Jina la kikoa.scot

Uskoti, (kwaKiingereza:Scotland ,Alba kwaKigaeli) , ninchi ndani yaUfalme wa Muungano, iliyoko katikaUlaya ya Kaskazini. Inapakana naUingereza kusini, na imezungukwa naBahari ya Kaskazini mashariki,Bahari ya Atlantiki kaskazini na magharibi, naBahari ya Ayalandi kusini-magharibi. Uskoti ina idadi ya watu takriban milioni 5.4, ikiwa ya 120 duniani. Mji wake mkuu niEdinburgh, huku jiji kubwa zaidi likiwaGlasgow. Uskoti imegawanyika katika maeneo 32 ya halmashauri. Inajulikana kwa urithi wake tajiri waKikelti naKigaeli, majumba ya kifalme yakihistoria, maeneo ya milimani (Highlands), na mchango wake mkubwa katikafalsafa,sayansi, na uhandisi wakati wa Enzi ya Mwangaza.

Jiografia

[hariri |hariri chanzo]

Uskoti nitheluthi ya kaskazini ya kisiwa cha Britania. Eneo lake nikm² 78,772. Upande wakusini Uskoti umepakana na Uingereza wenyewe.

Upande wamashariki kunaBahari ya Kaskazini, upande wa kaskazini namagharibi ile yaAtlantiki pamoja nabahari ya Eire.

Ndani ya nchi kuna kanda tatu:

Mlima mkubwa wa Uskoti niMlima Nevis karibu na Fort William wenyekimo chamita 1,344.

Mbali yabara Uskoti ina visiwa 790. Upande wa magharibi wa Uskoti bara likofunguvisiwa laHebridi. Upande wa kaskazini kunavisiwa vya Orkney navya Shetland.

Historia

[hariri |hariri chanzo]

Kihistoria Uskoti uliwahi kuwa nchi ya pekee, mpaka ikaunganishwa chini ya Ufalme waUingereza tangu mwaka1603BK.

Tangu mwaka1707 Uskoti haukuwa tena nabunge la pekee lakini ulikuwa na wawakilishi katika bunge laLondon.Bunge la Uskoti lilirudishwa tena mwaka1999 nalo linasimamia mambo ya ndani.

Mnamo Septemba2014, wananchi walipigakura kuhusuuhuru wa nchi yao, lakini wengi waliamua kudumisha Ufalme wa Muungano. Hata hivyo, baada ya Ufalme huo kujitoa katikaUmoja wa Ulaya, kuna mpango wa kupiga tena kura mwaka2023.

Miji kumi mikubwa ya Uskoti

[hariri |hariri chanzo]
MjiWakazi
5 Aprili 1991
Wakazi
29 Aprili 2001
Glasgow (Glaschu)658.379629.501
Edinburgh (Dùn Èideann)400.632430.082
Aberdeen (Obar Dhèathain)182.133184.788
Dundee (Dùn Dè, Dùn Dèagh)157.808154.674
Paisley (Paislig)73.92574.170
East Kilbride (Cille Bhrìghde an Ear)70.57973.796
Hamilton (Hamaltan)49.98848.546
Cumbernauld (Comainn nan Allt)49.50749.664
Greenock (Grianaig)49.26745.467
Ayr (Àir)47.96246.431

Picha za Uskoti

[hariri |hariri chanzo]

Viungo vya Nje

[hariri |hariri chanzo]
Nchi huru
Nchi zisizokubaliwa
na umma wa kimataifa
Maeneo yanayojitawala
chini ya nchi nyingine
1 nchi yaAsia ya Magharibi kijiografia ambayo huhesabiwa kuwa sehemu yaUlaya kiutamaduni2nchi ya kimabara
Makala hii kuhusu maeneo yaUlaya bado nimbegu.
Je unajua kitu kuhusuUskoti kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Uskoti&oldid=1421379"
Jamii:
Jamii iliofichwa:

[8]ページ先頭

©2009-2026 Movatter.jp