Usanisinuru unaanza kwenye sehemu za kijani za majani. Rangi ya kijani inatokana na punje ndogo sana zakiwiti ndani ya majani. Wakati nuru ya jua inafikia kiwiti inasababisha kemikali ndani yake kuvunja molekuli za maji. Molekuli ya maji ikivunjwa inatoa oksijeni,hidrojeni na nishati. Protini ndani ya seli inatumia dutu hizi pamoja na dioksidi kabinia ya hewani kujengaglukosi naATP ambayo ni molekuli yafosifati inayotunza nishati nyingi ndani yamuungo kemia wake.
Katika mchakato huu oksijeni inaachishwa na hivyo usanisinuru ni pia chanzo chaoksijeni katikaangahewa ya dunia jinsi ilivyo.
Makala hii kuhusu mambo yabiolojia bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuUsanisinuru kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.