Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Uranusi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uranusi
Picha yenye rangi halisi ya Uranusi kama ilivyoonwa na Voyager 2 mnamo 22 Januari 1986.
Picha yenye rangi halisi ya Uranusi kama ilivyoonwa naVoyager 2 mnamo 22 Januari 1986.
Ugunduzi
MgunduziWilliam Herschel
Tarehe13 Machi 1781
Jina
Asili ya jinaKla.Ūranus, kutokana naKgk. Οὐρᾰνός (Ouranós)
Alama♄
Tabia za mzunguko
Mkaribiokm 2,735,560,000
au 18.2861
Upeokm 3,006,390,000
au 20.0965
km 2,870,972,000
au 19.19126
Uduaradufu0.04717
siku 30,688.5
miaka 84.0205
Mwinamo0.773° tokanjia ya Jua
Miezi27
Tabia za maumbile
km 25,362±7
mara 3.976 ya Dunia
Tungamokg 8.6810×1025
mara 14.536 ya Dunia
g/cm3 1.27
Uvutano wa usoni
m/s2 8.69
km/s 21.3
siku −0.71832
siku −0.71833
Weupe0.300 (Bond)
0.488 (jiometri)
HalijotoK 76 (−197.2°C)

Kuhusu matumizi ya jinaZohali kwa sayari hii tazama kipengele cha "Asili ya jina"

Uranusi nisayari ya saba kutokaJua.

Asili ya jina

Waswahili wa kale hawakujua sayari hii. Uranusi ni jina la kimataifa lililoteuliwa katika karne ya 19 baada ya majadiliano marefu kati ya wanaastronomia wa Ulaya. Ni jina la mungu waUgiriki ya KaleUrano (Kgi.Οὐρανός) aliyeaminiwa kuwa mungu wa anga. Lugha nyingi duniani zimepokea jina hili kwa sababu astronomia ya zamani haikujua sayari hii.

Vitabu kadhaa vinatumia jina laKiswahiliZohali[1][2][3] kwa kufuata kamusi yaKAST; lakini hili ni jina la Kiswahili kwasayari ya sita (Kng.Saturn).[4]

Tabia

Ni sayari kubwa ya tatu yaMfumo wa Jua hata kama mada yake ni hasa gesi iliyoganda. Jumla ya masi yake ni mara 14 ya dunia hivyo ni sayari nyepesi kulingana na ukubwa wake. Kipenyo chake ni takriban kilomita 50,000[5].

Inazunguka Jua kwenye obiti inayochukua miaka 84. Umbali wake na Jua ni takriban mara 19 umbali wa Jua na Dunia aukilomita bilioni 2.9;afeli yake nivizio astronomia 20.11 naperiheli yake ni vizio astronomia 18.33.

Hadi mwaka 2023 miezi 27 iligunduliwa. Miezi mikubwa huitwaMiranda,Arieli,Umbrieli,Titania naOberoni. Ina pia pete kadhaa yaani mawingu ya vumbi, barafu na mawe madogo ambayo ni nyembamba na kuzunguka sayari kwa umbo la pete. Pete za Uranusi ni hafifu kuliko zile zaZohali.

Uranusi inaonekana kama nyota hafifu sana yenyemwangaza wa 5.6 - 6. Kutokana na kuwa hafifu vile na mwendo wake wa pole hakuna utamaduni wowote wa kale ulioitambua kuwa sayari. Ilitambuliwa mara ya kwanza kuwa sayari na tarehe13 Machi1781 naWilliam Herschel.

Tazama pia

Marejeo

  1. Wallah, W.B. & Mwamburi, J. Kiswahili mufti darasa la 8: Mwongozo wa mwalimu. Longhorn, 2009. ISBN 99966491066
  2. TESSA - Teacher Education in Sub Saharan Africa.Nishati na Mwendo: Kutoka Ardhini kenda kwenye nyota – kutumia Zana KifaniIlihifadhiwa 9 Aprili 2016 kwenyeWayback Machine.. Available at: www.tessafrica.net
  3. Waweru, M.; Makombo, H; Vonuoli, A.; Kashihiri, C.; Mwayani, J.Hutua za Kiswahili: Masomo ya Msingi 8. East African Educational Publishers ltd., 1ed, 290p., 2005.ISBN 9966-25-403-X
  4. KAST ni kamusi ya pekee inayotumia "Zohali" kwa sayari hii. Kamusi zaKKK/ESD yaTUKI naM-J SES zinaonyesha "Zohali" kwa sayari ya sita na "Uranus" kwa sayari hii. Linganisha ukurasa waMajadiliano:Sayari
  5. Uranus - by the numbers, tovuti ya NASA, iliangaliwa Januari 2021
Makala hii kuhusu mambo yasayansi bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuUranusi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Jua nasayari zake
Jua☉ Utaridi☿ Zuhura♀ Dunia🜨 Mirihi♂ Mshtarii♃ Zohali♄ Uranusi⛢ Neptuni♆
Sayari kibete
Seresi⚳ Pluto⯓ Haumea Makemake Erisi⯰
Kanda
Miezi mikubwa
Ganimedi Titani Kalisto Io Mwezi☾ Europa Tritoni
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Uranusi&oldid=1329185"
Jamii:
Jamii iliofichwa:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp