Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Upagani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Upagani nijina la kutajaimani zadini ambazo ama zinaabudumiungu mingi au nidini za jadi.

Neno hili linatumiwa hasa na watu katikamapokeo yaUkristo kutaja imani nyingine, lakini siku hizi, hasa katika nchi kadhaa zaUlaya, kuna pia vikundi vya watu ambao wanajiita hivi wenyewe.

Asili ya jina

[hariri |hariri chanzo]

Asili ya neno nilugha yaKilatini ambaPo "pagus" ni eneo lamashambani, mbali namiji mikubwa, na "paganus" nimtu anayeishi hukovijijini au mashambani.

Chaguo la neno hili kwa ajili ya dini kinatunzahistoria ya kwamba huko mwanzoni katika zamani zaRoma ya Kale Ukristo ulikuwa dini ya watu wa miji lakini imani za kale za Waroma ziliendelea kwa muda mrefu vijijini.

Istilahi

[hariri |hariri chanzo]

Hata kama neno "mpagani, upagani" linatoka katika mapokeo ya Kikristo, si lugha yaBiblia.

Maandiko yaBiblia ya Kiebrania kwa kawaida yanatumia neno "goi / goyyim" (גוי / גוים ) kwa kutaja watu wasioWayahudi. Goi inamaanisha "taifa" na mara chache inaweza kutumiwa pia kwa taifa laIsraeli.[1]. Lakini wingi wake "goyyim" (mataifa) unamaanisha watu wasio Wayahudi ambao pia wana imani tofauti.

KatikaAgano Jipya lugha hii imetafsiriwa kwaKigiriki na pale tunaposoma "mataifa"[2] kwaKiswahili lugha asilia yaKigiriki inatumia "ἔθνη, ethni"

Wapagani wapya

[hariri |hariri chanzo]

Tangukarne ya 19 kumekuwa na watu katika Ulaya waliotafuta njia mbadala za kidini nje ya Ukristo; wengine wao walijaribu kufufua imani za jadi za Ulaya na hapa wengine wametumia jina la "upagani" kwa imani hizi. Hao ambao wamekadiriwa kuwa makumi elfu katika nchi mbalimbali za Ulaya wanaitwa "neo pagans" yaani "Wapagani wapya"".

Tazama pia

[hariri |hariri chanzo]

Marejeo

[hariri |hariri chanzo]
  1. Kwa kawaida Biblia ya Kiebrania inatumia neno "am" kwa ajili ya Wayahudi wenyewe; "Am" ni kama "taifa" lakini zaidi kwa maana yaukoo ilhali "goy" ni taifa zaidi kwa maana ya kieneo na kisiasa.
  2. kama vile Luka 21, 24: Yerusalemu utakanyagwa na Mataifa
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Upagani&oldid=1018519"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2026 Movatter.jp