Niccolò Machiavelli ambaye, katika kitabu chabe maarufuThe Prince, aliandika kama kiongozi hawezi kuogopwa na kupendwa kwa wakati mmoja, ni afadhali aogopwe kuliko kupendwa.
Kipimo cha uongozi ni jinsi gani kiongozi anaweza kuletaushawishi kwa watu na kufikiamaendeleo yaliyotarajiwa.
Kiongozi bora hana muda wa kulalamika bali anatafutaufumbuzi wa matatizo ya wananchi au watu walio chini yake. Kiongozi wa kweli akiongea, watu husikiliza.
Uongozi nidhana,taaluma inayompa mhusikamadaraka nauwezo wa kuwawezesha wale wanaongozwa naye kuunganishanguvu,stadi na vipaji vyao na kuvitumia ili kufikia malengo yao. Kuongoza ni kujua lengo la wale wanaoongozwa na njia ya kufikia lengo lao.
Uongozi ni dhana, taaluma anayopewa mhusika katika kuwaongoza wale waliohitaji kusimamiwa au walioamuliwa kusimamiwa katika kufanikisha jambo fulani kwa maslahi ya wote au ya mtu mmoja mmoja.
iii.Uongozi wa kiimla ni mtindo wa kuongoza ambao kiongozi huongoza kwaamri bila kushirikisha watu wengine katika kufanya maamuzi. Mara nyingi uongozi wa aina hii haulengi katika kukidhimaslahi ya walio wengi, bali tu ya yule anayeongoza na wale wanaomlinda.
iv.Uongozi wa kidemokrasia ni ule wa kushirikisha watu katika kufanya maamuzi nautekelezaji wake. Kwa kawaida viongozi wa aina hii hulenga kukidhi mahitaji ya walengwa.
Viongozi wanaochaguliwa mara nyingi huwa wanapewa muda wa kuongoza, na wale viongozi wanaojiteua hujipatia wao wenyewe muda wa kuongoza au hata hapo watakapoamua kuachia madaraka.
i.Awe na ufahamu. Kiongozi ni lazima awe naufahamu mkubwa juu yataasisi anayoiongoza, malengo yake,mazingira na matatizo yake.
ii.Awe mwaminifu. Kila taasisi inalenga kufikiashabaha fulani. Niwajibu wa kiongozi kuwaongoza wanataasisi ili wafikie malengo yao. Kwa hiyo kiongozi ni lazima aweze kubuni mikakati nambinu zitakazoiwezesha taasisi anayoongoza kufikia malengo yake.
iii.Awe namaadili mema. Kiongozi ni lazima akubalike katikajamii na taasisi anayoiongoza. Ili akubalike hana budi kuzingatia maadili ya msingi ya jamii na taasisi yake. Mtu mwongo, mlevi, mvivu, asiye mwaminifu n.k. hawezi kuwa kiongozi mzuri.