Umoja wa Mataifa United Nations منظمة الأمم المتحدة 联合国 Organisation des Nations unies Организация Объединённых Наций Organización de las Naciones Unidas |
|---|
|
Nchi wanachama |
Mji mkuu na mkubwa | 760 United Nations Plaza, Manhattan, New York City (eneo la kimataifa) |
|---|
| Lugha rasmi | Kiarabu Kichina Kiingereza Kifaransa Kirusi Kihispania |
|---|
• Katibu Mkuu | António Guterres |
|---|
• Naibu Katibu Mkuu | Amina J. Mohammed |
|---|
• Rais wa Baraza Kuu | Philemon Yang |
|---|
• Rais wa Baraza la Kiuchumi na Kijamii | Bob Rae |
|---|
| Wanachama | 193 mataifa wanachama 2 mataifa waangalizi |
|---|
Historia |
• Kusainiwa kwa mkataba wa UM | 26 Juni 1945 |
|---|
• Mkataba ulifanyishwa kazi | 24 Oktoba 1945 |
|---|
| Jina la kikoa | .un |
|---|
Umoja wa Mataifa (UM) (Kiingereza:United Nations, UN) nishirika lakiserikali ambalo malengo yake ni kudumishaamani nausalama wa kimataifa, kuendeleza uhusiano wa kirafiki kati ya mataifa, kufikia ushirikiano wa kimataifa, na kuwa kituo cha kuoanisha matendo ya mataifa. Niumoja wanchi zoteduniani isipokuwa zile zisizotambuliwa kuwadola huru.
Umoja huo ulianzishwa na nchi washindi waVita Kuu ya Pili ya Dunia kuchukua nafasi yaShirikisho la Mataifa (1919 -1946). Makubaliano yalifikiwatarehe24 Oktoba1945 hukoSan Francisco,California.
Mwanzoni nchi zilikuwa 51 lakini kufikia mwaka2017 kulikuwa na nchi wanachama 193, mbali yaUkulu mtakatifu (Vatikani) naPalestina ambazo zinashiriki kamawatazamaji wa kudumu, zikiwa nahaki karibu zote isipokuwa kupigakura.
Dhumuni la umoja huu ni kuratibu mahusiano ya kimataifa kupitiasheria na mikataba ya kimataifa kwenye maeneo kamausalama,amani,maendeleo ya jamii na yauchumi,haki za binadamu,uhuru,demokrasia n.k.
Toka mwanzomakao makuu ya Umoja wa Mataifa yakoManhattan,New York City,New York nchiniMarekani na hayako chini yamamlaka ya nchi hiyo.Ofisi nyingine zikoGeneva (Uswisi),Nairobi (Kenya) naVienna (Austria).
Lugha rasmi za UM nisita:Kiarabu,Kichina,Kifaransa,Kihispania,Kiingereza naKirusi.
Katibu Mkuu wa UM anachaguliwa kwa miaka mitano; kwa sasa niAntónio Guterres kutokaUreno, aliyechaguliwa kuwa Katibu Mkuu mwaka2016 akichukua nafasi yaBan Ki-moon.