Umoja wa Kilatini (kwaKilatini:Unio Latina; kwaKiingereza:Latin Union) ni shirika la kimataifa linalounganisha nchi mbalimbali zinazotumia rasmilugha za Kirumi. Umoja huo ulianzishwa mnamomwaka1954 kamamkataba wa kimataifa na tangu mwaka1983 ulikuwataasisi halisi yenyeofisimjiniParis. Ofisi kuu ilifungwa tena mnamo mwaka2012 kwa sababu wanachama wengi hawakulipaada zao.
Makao yake makuuyalikuwa Paris,Ufaransa, lengo lake lilikuwa kulinda na kukuzaurithi wakitamaduni wamataifa yenye lugha za Kirumi.Idadi ya wanachamama ilifikia nchi 36 zaAmerika Kaskazini,Amerika Kusini,Ulaya,Afrika, na kanda laAsia naPasifiki.[1]
Majina rasmi ya Umoja wa Kilatini yalikuwa: Union Latine kwaKifaransa, Unione Latina kwaKiitalia, Uniao Latina kwaKireno, Uniunea Latina kwaKiromania, Union Latina kwa Kihispania na Unio Llatina kwaKikatalunya.