Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Ulaya ya Mashariki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ulaya ya Mashariki ni sehemu yamashariki yabara laUlaya lakini hakuna maelewano juu ya mipaka yake hasa upande wamagharibi.

Ulaya Mashariki kutokaangani.

Ulaya ya Mashariki kufuatana na Umoja wa Mataifa

[hariri |hariri chanzo]

Umoja wa Mataifa hujumuisha nchi zifuatazo humo:

Orodha hii imejumlisha nchi zote za Ulaya zilizokuwa sehemu zaUmoja wa Kisovyeti au zilizoshikamana nao kisiasa hadi mwaka1989 (isipokuwaUjerumani ya Mashariki). Tatizo lake ni ya kwamba watu wa Polandi, Hungaria, Ucheki na Slovakia zinajihesabu kuwa sehemu zaUlaya ya Kati.

Ukuaji wa Ukristo Ulaya.

Ulaya ya Mashariki kijiografia

[hariri |hariri chanzo]

Kijiografia mara zinatajwa humo nyingi nchi zaUkraine,Belarus,Moldova na sehemu ya Ulaya waUrusi. Isipokuwa sehemu za kaskazini za Urusi huhesabiwa mara nyingi upande waUlaya ya Kaskazini.

Ulaya ya Mashariki kiutamaduni

[hariri |hariri chanzo]

Mara nyingi nchi zinazokaliwa na watu wenyelugha za Kislavoni huhesabiwa humo. Lakini kwa njia hii Romania na Hungaria si nchi za Ulaya ya Mashariki lakini Ucheki,Slovenia naKroatia zimo. Kihistoria hata sehemu zaUjerumani zilikaliwa naWaslavoni, naWasorbi katika mashariki bado hutumialugha yao.

Hivyo kuna nji ya pili inayosema: Nchi zote zenye lugha za Kislavoni zilizoguswa hasa naKanisa la Kiorthodoksi kama vile Urusi, Ukraine, Belarus.

Ulaya portal
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Ulaya_ya_Mashariki&oldid=1427314"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2026 Movatter.jp