Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Ukristo katika karne za kwanza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
     Uenezi wa Ukristo hadi mwaka 325     Uenezi wa Ukristo hadi mwaka 600
Sehemu ya mfululizo kuhusu
Ukristo
Yesu Mchungaji mwema.

Ukristo katika karne za kwanza ni sehemu yahistoria ya Kanisa hadimwaka325BK, ulipofanyikamtaguso mkuuwa kwanza hukoNisea, leo nchiniUturuki.

Kwa kawaidakarne hizotatu zinagawiwa pandembili: wakati waMitume wa Yesu (hadi mwaka100 hivi) na baada yakifo chao wote.

Wakati wa Mitume

[hariri |hariri chanzo]

Habari kuu za kipindi cha kwanza, kama ile yasiku yaPentekosteRoho Mtakatifu kuwashukia wafuasi waYesu, zinapatikana hasa katikaMatendo ya Mitume,kitabu kilichoandikwa namwinjili Luka kwenyemiaka ya 80. Humo unasimuliwa hasauenezi waUkristo katika maeneo ya upande wakaskazini waBahari ya Kati.

Tukio lingine muhimu linalosimuliwa na Luka niuongofu waMtume Paulo, mwenezi mkuu wa Ukristo namfafanuzi bora waimani hiyo mpya.[1]

Pamoja na uenezi, linajitokeza badiliko kubwa laWakristo: awali walikuwa woteWayahudi ama kwa kuzaliwa ama kwa kuongoka,[2] nao wanaitwaWakristo wa Kiyahudi. Lakini katikakarne ya 1 tayariidadi yao ilizidiwa na ile ya Wakristo wamataifa mengine.

Sambamba na hilolughaya kimataifa yaKigiriki ilizidi kutumika badala yaKiaramu,lugha mama ya Yesu na mitume wake.[3] Ndiyo sababuAgano Jipya limeandikwa lote kwa Kigiriki. Vitabu 27 vinavyoliunda vilianza kulinganishwa na vile vyaAgano la Kale kama vitakatifu.

TenaYerusalemu, uliokuwamji mkuu waWayahudi na waWakristo wa kwanza, ulizidi kukosa umuhimu, hasa baada yaMtume Petro na wenzake kuuhama au kuuawa. Wakati wavita vya kwanza vya Kiyahudi hata waumini wa kawaida walihama, na waliporudi hakukuwa tena nahekalu, kwa kuwa lilibomolewa mwaka70. Mbali ya hayo, uhusiano na Wayahudi ulizidi kuharibika, na hatimaye Wakristo walikatazwa wasishiriki tena ibadasinagogini.

Jumuia yaRoma,makao makuu yadola, ilizidi kuwa muhimu, hasa baada ya kufikiwa na Petro na Paulo, ambao walimalizia hukokazi yao kwakufia dini katikadhuluma ambayo ilianzishwa naKaisari Nero mwaka64 na kuendelea kwakwikwi hadi mwaka313.

Wakati wa watetezi wa imani

[hariri |hariri chanzo]

Bila kujalidhuluma hiyo ya nyingine, Ukristo ulizidi kuenea ndani na nje yaDola la Roma.

Ushujaa waumati wawafiadini naupendo kati ya Wakristo vinafikiriwa kuwa sababu kuu ya uenezi. Kutoka kwenyemiji, imani ilizidi kueneavijijini pia.

Pamoja na hayo, walianza kujitokezawaandishi mbalimbalikuteteaKanisa mbele yaserikali, na wengine kuchambuaimani dhidi yauzushi uliozidi kupata nguvu hasa kwa namna yaGnosis. Waandishi hao ni kati ya wale wanaoitwa mababu wa Kanisa au walau waandishi wa Kikanisa.

Wakati huohuo matumizi ya vitabu vya Agano Jipya katika ibada yalizidi kujadiliwa na kutungiwaorodha rasmi (Kanuni ya Biblia).

Tanbihi

[hariri |hariri chanzo]
  1. Oxford Dictionary of the Christian Church ed. F.L. Lucas (Oxford) entry on Paul
  2. Catholic Encyclopedia: Proselyte: "The English term "proselyte" occurs only in the New Testament where it signifies a convert to the Jewish religion (Matthew 23:15; Acts 2:11; Acts 6:5; etc.), though the same Greek word is commonly used in theSeptuagint to designate a foreign sojourner in Palestine. Thus the term seems to have passed from an original local and chiefly political sense, in which it was used as early as 300 B.C., to a technical and religious meaning in the Judaism of theNew Testament epoch."
  3. Ehrman, Bart D. (2012).Did Jesus Exist?: The Historical Argument for Jesus of Nazareth. HarperCollins, pp 87- 90.

Marejeo

[hariri |hariri chanzo]

Marejeo mengine

[hariri |hariri chanzo]
  • Pelikan, Jaroslav Jan (1975).The Christian Tradition: The Emergence of the Catholic Tradition (100–600). Chicago: University of Chicago Press.ISBN 978-0-226-65371-6.
  • Stark, Rodney (1997).The Rise of Christianity. New York: HarperCollins.ISBN 978-0-06-067701-5.
  • Taylor, Joan E. (1993).Christians and the Holy Places: The Myth of Jewish-Christian Origins. Oxford: Oxford University Press.ISBN 978-0-19-814785-5.
  • Thiede, Carsten Peter (2003).The Dead Sea Scrolls and the Jewish Origins of Christianity. Basingstoke: Palgrave Macmillan.ISBN 978-1-4039-6143-3.

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuUkristo katika karne za kwanza kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Ukristo_katika_karne_za_kwanza&oldid=1456164"
Jamii:
Jamii iliofichwa:

[8]ページ先頭

©2009-2026 Movatter.jp